Sunday 19 February 2017

Bangi yasababisha Polisi wanane kutimuliwa Kazi

Baada ya Mahakama ya Kijeshi kuwatia hatiani polisi wanane mkoani Kilimanjaro kwa kukamata magunia 10 ya bangi na kuyaachia, wamefukuzwa kazi.
Tukio hilo la polisi kukamata bangi hiyo, lilitokea Oktoba mwaka jana likihusisha askari wa Kituo cha Polisi Sanyajuu wilayani Siha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kuchukua hatua hizo baada ya kuridhika na tuhuma dhidi yao.
“Ni kweli kama ulivyopata hizo taarifa. Nimechukua uamuzi huo baada ya kuthibitishwa walikamata magunia 10 ya bangi na kuyaachia. Yule mkaguzi suala lake tumelipeleka juu,” amesema.
Polisi waliofukuzwa kazi kwa fedheha ni Sajenti Sadick D.6004, Koplo Innocent (D.9830), Koplo Deusdedit (E.1703), Koplo Semu (E.7525), Koplo Salum (E.8907), PC Kiroga (F.8983), PC Filbert (F.8385) na PC Ramadhan (G.3222).

from Blogger http://ift.tt/2kAXW4U
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2kB6rwJ

No comments:

Post a Comment