Monday, 20 February 2017

Mr. T Touchez amleta rasmi Harmorapa

Zikiwa zimepita wiki mbili sasa tangu rapa anayechipukia Harmorapa kukutana na producer anayefanya vyema kwa sasa kwenye sekta ya muziki Mr. T Touchez na kufanya kazi pamoja inasemekana kazi ya rapa huyo iko tayari kwenda mtaani hivi sasa.
Producer T Touchez amefunguka na kusema kazi hiyo imekamilika kila kitu na sasa ipo tayari kwenda kwa wananchi ili waweze kumsikia rapa huyo ambaye baadhi ya watu wanatilia shaka kuwa hawezi muziki, huku wengine wakimpa moyo kuwa akaze atatoka kwenye muziki na kufanikiwa kama watu wengine.
“Harmorapa final mix niambie hii nyimbo niitoe lini? “. Alihoji Mr T Touchez 
Awali Mr. T Touchez alipokutana na Harmorapa alimpa ushauri kuwa aache maneno bali anatakiwa kuleta muziki mzuri ili kuweza kukata ngebe za baadhi ya watu ambao huenda hawaamini katika uwezo wake. 
Harmorapa mpaka sasa ni kati ya wasanii wachache ambao wanachipukia na kuweza kuwa na kismati cha kupendwa na watu wa lika zote kutokana na namna anavyoishi na jinsi ambavyo yeye mwenyewe anajiweka.
Hadi sasa amefanikiwa kukutana na watu wengi maarufu akiwemo Producer nguli wa muziki wa bongo fleva P Funk Majani, Juma Nature, na Erick Shingongo ambao wote walionyesha kufurahi kukutana na kijana huyo. 
Harmorapa alipotembelea Mkurugenzi wa Global Publishers, Erick Shingongo ofisini kwake

from Blogger http://ift.tt/2lmpuYx
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2kQ9s7t

MAAJABU : Tazama VIDEO ya Kijana Aliyetengeneza GARI huko Mwanza kwa Kutumia Vifaa vya Baiskeli

Tanzania ni nchi ambayo imekuwa nyuma sana kiteknolojia, sio viwanda vya kutengeneza hata pipi, toothpick nk vimekuwa ni adimu na vitu vingi tunavyotumia vimekuwa vikiagizwa nje ya nchi… Kama hilo halitoshi, vijana wanaoonyesha jitihada za kubuni vitu mbalimbali vya kiteknolojia wamekuwa hawapewi sapoti inayostahili…. Mfano ni kijana huyu aishiye mwanza wilaya ya Kwimba, Ameweza kutengeneza Gari kwa kutumia vifaa vya baiskeli na linatembea barabarani. Tazama Video Hapa chini

from Blogger http://ift.tt/2kDEiFb
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2me92c3

Wanasheria wa CHADEMA Wamtaka Mbowe Asijisalimishe Polisi

Wanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamesema wamemshauri Mwenyekiti wao wa Taifa, Freeman Mbowe, asiende kuripoti polisi leo.
Mwanasheria wa Chadema, John Mallya, amesema Mbowe hatakwenda kuripoti polisi leo kwa sababu amefungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam na inaanza kusikilizwa Februari 21 mwaka huu.
“Mbowe haendi polisi, tumemshauri asiende kwa sababu kesi yake inaanza kusikilizwa Jumanne (kesho).
“Kama wanamhitaji, waje keshokutwa (kesho) Mahakama Kuu, watampata hapo,”alisema Mallya.
Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, alisema yuko Mwanza na hajawasiliana na Mbowe.
“Hapa niko Mwanza sijawasiliana na mwenyekiti, lakini kama nikiwasiliana naye, nitamshauri asiende huko polisi.
“Kwa hiyo, naweza kusema kilichofanywa na Kamishna Sirro si wito wa kipolisi bali ni siasa kama ambavyo alifanya Makonda kwa kutangaza majina ya watu hadharani.
“Wito wa polisi huwa ni wa kimaandishi, hawajamwandikia barua, hawajampigia simu.
“Hawa maafande wana namba zetu za simu sisi kama mawakili wa chama, kama wanamhitaji Mbowe kwanini wasitupigie simu mpaka watangaze kwenye vyombo vya habari,”alihoji Lissu.
Alipoulizwa kama Mbowe atakamatwa wakati wowote kuanzia sasa, Lissu alisema watalazimika kulishtaki mahakamani Jeshi la Polisi kwa kitendo hicho.
“Hatuwezi kukubali utaratibu huu, waache kufanya siasa, wakimhitaji mwenyekiti wetu wamwandikie barua,”alisema Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki.
Mwanzoni mwa mwezi huu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alitaja majina 65 ya watu wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya akiwamo Mbowe.
Pamoja na kutaja majina hayo, Makonda aliwaagiza watuhumiwa hao kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa dhidi ya tuhuma hizo.
Februari 10 mwaka huu, akiwa mjini Dodoma, Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, alizungumza na waandishi wa habari na kusema hajawahi kujihusisha kwa namna yoyote na biashara ya dawa za kulevya na pia hatakwenda polisi kuhojiwa kama alivyoagizwa na Makonda.
Hata hivyo, alisema atakwenda polisi, kama jeshi hilo litafuata taratibu za kumuita kwa mujibu wa sheria.
“Siwezi kwenda polisi kwa wito wa Makonda kwa sababu hana mamlaka hiyo kisheria. Kama polisi wananihitaji, waniite kwa kufuata utaratibu, nitakwenda kwa sababu mimi siogopi kwenda polisi,”alisema Mbowe.
Wakati Mbowe akisema hayo, juzi Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, alisema Jeshi la Polisi linamtafuta Mbowe na kwamba limeshindwa kumpata kwa sababu amezima simu.
Kutokana na hali hiyo, Kamanda Sirro alitoa saa 48 kwa Mbowe kuripoti polisi na endapo hatafanya hivyo atatafutwa kwa namna ambayo jeshi hilo litaona inafaa.
“Jumatatu (leo) asiporipoti kutakuwa hakuna namna ya kulizuia tena Jeshi la Polisi kutafuta namna ya kumhoji.
“Mbaya zaidi juzi tumejitahidi kumtafuta hapatikani, tulikwenda nyumbani kwake hakupatikana, tulikwenda mahali anakoishi sasa, pia hakupatikana,”alisema Sirro

from Blogger http://ift.tt/2lCkgur
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2kQ1JXf

Jumuiya ya Kiisilamu yataka MATEJA Wote washtakiwe na Pia Mali za Paul Makonda Zichunguzwe

Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini imevitaka vyombo vya kisheria na uchunguzi kuacha kupuuza kauli zilizotolewa na wabunge zilizomtuhumu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumiliki mali zisizoendana na kipato chake halali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Msemaji wa Jumuiya hiyo Sheikh Rajabu Katimba, alisema wakati wa mkutano wa Bunge lililopita baadhi ya wabunge walimtuhumu Makonda hivyo tuhuma hizo zinapaswa kufanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria.
Alisema vyombo vyenye mamlaka ya uchunguzi vinapaswa kufanya uhakiki wa mali za Makonda ili kuondoa shaka katika umiliki wa mali aliyonayo na uhalali wa misaada ya kifedha zinazotolewa kwake na taasisi rafiki.
Sheikh Katimba alisema kifungu cha (11) cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma inamtaka kiongozi kutaja hadharani mali zake ikiwemo zawadi anazopewa.
Hivi karibuni, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) wakati akichangia taarifa za Kamati ya Bunge na Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama alisema Makonda amenunua jengo ‘(Apartment ) lenye thamani ya shilingi mil 600 jijini Dar es Salaam.
Selesini aliliambia Bunge kuwa Makonda amempa gari mkewe aina ya Mercedez Benzi lenye thamani ya Dola 250,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh milioni 550.
Mbali na Selesini, Mbunge mwingine aliyemtuhumu Makonda kujilimbikizia mali ni Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma (CCM) ambaye naye wakati akizungumza bungeni alihoji ni wapi Makonda alipata fedha za kusafiri kwenye ndege daraja la juu kwenda Marekani.
Wakati huo huo, Sheikh Katimba alisema vita dhidi ya dawa za kulevya inaweza kwenda vibaya iwapo itasimamiwa na wanasiasa.
Alisema ili kuepuka hilo vyombo vya dola vyenye mamlaka ya kisheria vinapaswa kuifanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa.
Sheikh Katimba alisema taasisi za kiislamu zinaunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali kupambana na biashara hiyo na kusisitiza kuwa vyombo vyenye mamlaka kuisimamia kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya nchini ya mwaka 2014.


‘’Hatuoni ni kwa mantiki ipi watumiaji wengine washitakiwe kwa kutumia dawa na wengine waachiwe huku zitumike na fedha za kuwatibia nje ya nchi.

‘’Wasanii kama Rehema Chalamila, maarufu kwa jina la Ray C’ msanii TID nao pia walipaswa kushitakiwa kama walivyofanywa wengine na vilevile watumiaji walioko mitaani na kwenye vituo vya daladala wote wasombwe wakapimwe na kisha washitakiwe.

“Pamoja na nia ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuongoza na kuendesha vita hiyo lakini vita isimamiwe na vyombo vyenye weledi na si wateule wa kisiasa au wanasiasa,’’ alisema.

Aidha, alizungumza kesi za ugaidi inawakabili baadhi ya viongozi wa dini kwa kueleza kuwa haitakuwa na tija wala heshima iwapo viongozi hao wataendelea kushikiliwa gerezani.

“Ni kweli serikali inatutaka tuiunge mkono kwenye vita hiyo nasi tuko tayari lakini ni vuziri jitihada hii ikawa kwa watu wote, tunaiona serikali inashindwa kutenda haki kwa viongozi wa dini yetu na ni kesi gani isiyokwisha? inatia aibu masheikh kufungwa bila hatia miaka mitatu ni sawa na kufungwa bila hatia,’’ alisema Sheikh Katimba.

from Blogger http://ift.tt/2lC8S1v
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2kZacYJ

Mzee wa Upako Afunguka Kuhusu yeye Kunywa Pombe…..Atangaza Maamuzi Mapya Kwa Waandishi Aliowatabiria Kifo.

Mchungaji Anthony Lusekelo amefunguka kuhusu tuhuma za yeye kunywa pombe, na kuweka wazi kuwa hanywi pombe bali anakunywa ‘wine’ isiyo na kilevi, huku akisita kusema endapo unywaji pombe ni dhambi au siyo dhambi.
Amefunguka hilo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI cha EATV, na kuweka wazi kuwa wanaomtuhumu kuwa yeye anakunywa pombe wanapaswa kutoa ushahidi juu ya tuhuma hizo, na kwamba unywaji pombe unaweza kuwa dhambi ama usiwe dhambi kulingana na imani na dini ya mtu.


“Hao wanaotuhumu kuwa nakunywa pombe, waeleze ni pombe gani nakunywa, nilikuwa nakuywa wapi na aliyeniona ni nani… kuna sehemu nyingine pombe siyo dhambi, dini nyingine mpaka kanisani kuna bar”.

Je, kunywa bia kiasi bila kulewa ni dhambi au siyo dhambi?
Hilo ni swali lingine alilokutana nalo kuhusu unywaji Pombe, ambapo katika majibu yake amesema hawezi kusema kama ni dhambi au lah, maana inategemea na imani ya mtu, huku akiongeza kuwa Bibilia haijazuia unywaji pombe

“Inategemea na makanisa, kuna mengine hata kunywa soda ni dhambi. Dhambi ni makubaliano yenu kwenye dini yenu. Bibilia inasema kula kitu chochote hata chakula kama ukila kupitiliza ni dhambi, hata unywaji wa pombe ukinywa ukapitiliza ni dhambi. Biliblia haijaandika moja kwa moja kwamba msinywe pombe, imesema msilewe kwa kuwa ndani ya ulevi kuna ufisadi, cha msingi mbadilishe ulevi wenu uwe ni roho mtakatifu”

Ikumbukwe kuwa sekeseke lililosababisha Mzee wa upako adaiwe kunywa pombe, lilihusisha kurushiana maneno na jirani zake ambapo baada ya hapo vyombo vya habari hasa magazeti yaliripoti tukio hilo kwa namna ambayo Mzee wa Upako hakuipenda, na hata kufikia hatua ya kuwatabiria kifo waandishi walioandika habari hiyo.
Alipoulizwa kuhusiana na ahadi yake hiyo ya kuwatabiria vifo, alisema kuwa tayari amewasamehe ingawa uwezo wa kuwaombea kifo anao.

“Tulisema hatuwezi kutumia nguvu kubwa sana kuwaombea watu kifo, kwa sababu sisi ni wanadamu, na wanadamu tuna mapungufu kwahiyo nikaona ni bora kumuachia Mungu. Uwezo huo wa kuwaombea watu wakafa, mimi ninao, lakini nikaona inasaidia nini mtu kumuombea mabaya, kwahiyo nikaamua kusamehe”

Baadhi ya watu walitaka kujua ni kwanini haendi kuombea wagonjwa hospitalini ili wapone, ambapo alijibu kuwa maombi hufanywa katika mazingira maalum, na kwamba hospitali kila mgonjwa ana imani yake.


“Maombi lazima kuandaa mazingira, na sehemu ambayo Mungu amesema tukutane ni kanisani, ndiyo maana hata wakati wa Yesu wagonjwa ndiyo walimfuata Yesu, siyo Yesu aliwafuata wagonjwa.. Kinachoponya ni imani ya mtu, pale hospitali kila mtu ana imani yake, wakati mwingine hata kumuombea mtu inabidi umuombe kwanza maana wengine hawapendi kuombewa”

from Blogger http://ift.tt/2kPYAXr
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2lCiucM

Video:Gigy aeleza kisa cha kugombana na Mo J, ‘alichepuka na mimi nikachepuka ajue maumivu yake’

Mtangazaji wa kipindi cha Lavidavi cha ChoiceFm, Gigy Money amefunguka kwa kueleza kilichosababisha akagombana na mpenzi wake Mo J na jinsi walivyomaliza ugomvi wao.
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Gigy amedai aliumizwa na kitendo cha kupigwa na mpenzi wake huyo baada ya kugundua amechepuka.
“Kuna mambo yalitokea, Mo J alichepuka mimi nikamshtukia, kwa baada ya kumwambia akaanza kunigiga,” alisema Gigy Money.
“Lakini namshukuru mungu yameisha baada ya mimi pia kuchepuka, kwa sababu labda alikuwa hajui maumivu ya kuchepuka, kwahiyo sasa hivi tupo sawa,”

from Blogger http://ift.tt/2m0807G
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2lC27Ne

MAMA ATIWA MBARONI KWA KUMPAKA PILIPILI MACHONI MTOTO KISA HAJAFUA NGUO ZA SHULE

Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la ‘Mama Saidi’ anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuwekea pilipili kwenye macho mtoto wake wa kambo anayesoma darasa la sita kwa madai ya kutofua nguo za shule.
Tukio hilo limetokea Mtaa wa Tabata Magharibi na kuripotiwa kwenye ofisi ya Serikali ya Mtaa huo juzi, kabla ya mwanamke huyo kukamatwa na kupelekwa Kituo cha Polisi Tabata ambapo anashikiliwa hadi sasa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Amaduni alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema upelelezi bado unaendelea.
“Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika, ikiwa ni pamoja na kupokea taarifa ya daktari ambayo itaonyesha ni kwa kiasi gani mtoto huyo ameumia au madhara aliyoyapata kutokana na kitendo kile,” alisema Amaduni na kuongeza:
“Bado tunakusanya ushahidi, ukikamilika tutapeleka jalada kwa mwanasheria wa Serikali kwa hatua za mashtaka.”
Awali majirani walidai imekuwa kawaida kwa mwanamke huyo kumnyanyasa mtoto huyo wa kambo, lakini Kamanda Amaduni alisema tukio hilo ni la kwanza kuripotiwa kutoka kwa mwanamke huyo na si kama wanavyoeleza majirani zake.
Mtendaji wa mtaa huo, Hamza Ramadhani alisema mtoto huyo alipofikishwa ofisini kwake alikuwa haoni kutokana na athari za pilipili, ndipo alipopelekwa Kituo cha Afya Tabata.
“Lakini walipomuangalia waliamua kumpeleka Hospitali ya Amana na taarifa nilizanazo kwa sasa jana(juzi) amesharuhusiwa yupo nyumbani na mwenzake ila mama ndio bado yupo polisi,” alisema.
Jirani wa mtoto huyo, Gowely Anthoy alisema kwa kipindi kirefu kulikuwa na viashiria vya mtoto huyo kunyanyaswa lakini hakuna aliyeweza kuhoji.
“Mtoto mwenyewe amekuwa akisema tangu siku nyingi mama hamhudumii ipasavyo, lakini tulikuwa tukichukulia kama masuala ya kawaida ya watoto, lakini sasa tumejua ni kweli,” alisema.

from Blogger http://ift.tt/2m07qXx
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2m01P3h