Sunday 19 February 2017

Mwanaume alazimika Kuishi na Maiti ya mama Yake Ndani

Marehemu Bi Henderika Apondi Were (aliyeashiriwa pichani).
MWANAMUME amelazimika kuishi na jivu la maiti ya mamake baada ya kukosa nauli ya kusafirisha jivu hilo hadi kaunti ya Siaya nchini Kenya.
Kulingana na Samson Were, 25, Bi Henderika Apondi Were ambaye ni mamake mzazi aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 45 baada ya kugongwa na gari la moshi nchini Ujerumani Septemba 2016.
“Mama alikuwa amekatwakatwa na gari la moshi kwenye ajali hiyo nikasema achomwe manake alikuwa vipandevipande alipozolewa. Walihifadhi mabaki ya mwili wake na kusafirisha hadi humu nchini,” akasema.
Kijana huyo alisema aliandikiwa barua na rafiki ya mamake ili atie saini kwamba hatopigania wala kufuatilia mali ya mamake huko Ulaya; ingawa alikataa kutia saini barua hiyo iliyotumwa kieletroniki.
Mama huyo aliolewa na Mjerumani Stephan Gronert jijini Nairobi Julai 5, 1994.
Kulingana na mwanawe Bi Apondi, baada ya ndoa wawili hao walisafiri nchini Ujerumani baada ya wiki moja.
Mumewe alifariki baada ya kuhusika kwenye ajali mwaka 2011.
“Huyu baba naye aligongwa na treni akafa. Mamangu ananisumbua na ndoto anataka kuzikwa bara lakini sina namna, mama anataka kuzikwa kwa shamba lake huko Siaya. Nataka nimzike kwa shamba letu mahali nitajenga,” akasema.
Alisafirishwa nchini Februari 3, 2017.
Sanduku
Were alisema ananuia kununua sanduku la futi nne ambapo ataweka jivu la mamake.
“Nikishaweka jivu sandukuni nitaweka nguo nyeupe, Nitanunua nguo ambayo nitamzika nayo. Nitamzika kama vile mtu wa kawaida anafaa kuzikwa,”akasema.
Were ameitaka Wizara ya Maswala ya kigeni kuhakikisha inafuatilia kifo cha mamake.
“Mama alikuwa ameniambia atanitumia Sh10 milioni nianze kufanya biashara lakini kesho yake nikapigiwa simu na rafiki yake kuwa amegongwa na gari la moshi. Ninashuku sana kifo chake. Isitoshe tunataka serikali ifuatilie mali aliyoiacha manake sisi hatuna namba,” akasema Were.
Alisema wajomba zake walizika mgomba kama mila za Kijaluo Oktoba 2016 huko Samia, Busia.

from Blogger http://ift.tt/2lX9ZJM
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2mbm627

No comments:

Post a Comment