Sunday 19 February 2017

Maiti zazikwa Juu ya zingine jijini DSM

Hali ya Jiji la Dar es Salaam katika kipindi hiki inakabiliwa na maeneo mengi ya makaburi kujaa, hasa ya katikati ya mji na yale yaliyo katika halmashauri za wilaya.
Likiwa na idadi ya watu milioni 4.36 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, linapokea watu wengi kutoka maeneo mengine kiasi cha kufanya wastani wa ongezeko la watu kuwa asilimia 5.6.
Katika baadhi ya maeneo maarufu ya Kisutu, Kinondoni, Sinza, Chang’ombe, Wailes, Buguruni na Ubungo, maiti zinazikwa juu ya zile zilizofukiwa awali.
Maeneo ya katikati ya jiji kama Kisutu na Kinondoni ndiyo yamekithiri kwa maiti kuzikwa juu ya nyingine, na hata ule utamaduni wa ndugu kushiriki kuchimba makaburi sasa unapotea kutokana na wachimbaji kuchelea kuruhusu watu wengine kushuhudia shughuli hiyo.
Meya wa Ubungo, Boniface Jacob alipozungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani, amesema maeneo ya makaburi maarufu kama Sinza Makaburini, Ubungo na Kibo yanayotegemewa na manispaa hiyo, yameshajaa.
“Ubungo pamoja na wakazi wake kuwa wengi, kuna sehemu tatu maarufu za kuzikia; Sinza, Ubungo Maziwa, Kibo na Kimara na zimeshajaa. Sasa huko kote inabidi tufunge na kutafuta maeneo mapya ya kufanya shughuli za mazishi isiwe kuzika marehemu juu ya marehemu,” amesema Jacob.
Chanzo: Mwananchi

from Blogger http://ift.tt/2kM3HYx
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2kB6dWt

No comments:

Post a Comment