Je ungependa kupata tena vitu ulivyofuta kwa bahati mbaya au umefuta lakini imetokea dharura na unavihitaji tena?. Usiwaze tena, kuwa huru kufuta kitu chochote kama vile video, audio, picha, document n.k kwani unaweza kuvirudisha endapo utavihitaji tena. Kama ilivyo kwenye computer (Recycle Bin), Dumpster ni android App ambayo inahifadhi mafile yote yanayofutwa kwenye simu ambapo unakuwa na nafasi nyingine ya kurudisha (Restore) mafile au vitu hivyo.
Jinsi ya kuipata, nenda playstore kisha tafuta “Dumpster” na install au bofya hapa kuipata Kutoka Playstore.
Jinsi ya kurudisha files
Kabla hujafuta file lolote hakikisha umeifungua Dumpster na iko active. Ikiwa umefuta files na unahitaji kulirejesha fuata hatua hizi;
1. Fungua Dumpster kisha chagua file unalotaka kurudisha
2. Baada ya kuchagua file, bofya “restore” kama inavyoonekana hapo chini. Tayari utakuwa umerudisha file lako. Unaweza ukachagua kufuta moja kwa moja kwa kubofya delete
Kumbuka, Dumpster inarudisha mafaili yaliyofutwa ikiwa tayari ilishakuwa installed, mafaili yaliyofutwa kabla ya kuinstall Dumpster hayatoweza kurudishwa kwa kutumia App hii. Pia unashauriwa kufuta moja kwa moja mafile ambayo unahisi huyahitaji tena ili kuongeza nafasi kwenye simu yako.
from Blogger http://ift.tt/2meYR7b
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2lzho0R
No comments:
Post a Comment