Monday, 20 February 2017

Zifahamu Sababu Na Namna Ya Kuzuia Smartphone Yako Kupata Moto

Kama Simu Yako Itaanza kupata Joto pindi uitumiapo ni Jambo la kuwa nalo makini kwani Husababisha Smartphone yako Kuisha Chaji Mapema na Pia Huweza Kusababisha Simu Kulipuka Endapo Joto Litazidi.
SABABU ZINAZOPELEKEA SMARTPHONE KUPATA JOTO
  • -Kuifanyisha simu kazi nyingi kwa muda mrefu. Mfano kudownload Vitu Mtandaoni, huku ukiangalia Muvi au hapohapo ukicheza Gemu katika simu yako.
  • -Joto kali katika Mazingira Yanayokuzunguka. kuwa muangalifu Simu yako inapokuwa Juani kwa Muda Mrefu.
  • -Kava Lililo Funika Simu Yako Huenda Halipitishi hewa ya kutosha Hivyo kusababisha Simu Kukusanya Joto.
  • -Matatizo ya Betri na Chaja Husababisha Simu Kupata Joto. Endapo Unatumia Betri Iliyokwisha Choka au betri ambayo Sio Halisi Kwa ajili ya simu Yako Husababisha Smartphone yako Kupata Joto.
  • -Kupiga Simu Au Kupoke Simu Pindi Smartphone Yako Inapochajishwa. Hii itakuweka hatarini kulipukiwa na simu Sikioni.
  • -Kuweka Software ambazo haziendani na simu yako. Baada ya Ku’Root’ Smartphone yako Unawezakujikuta Umeweka Software ambazo zitaipa shida simu yako Bila ya wewe kujijua.
  • -Matumizi ya internet kwa Muda Mrefu. Internert ni Moja vtu vinavyotumia Kiwango kikubwa cha nguvu ya Prosesa ya simu Hivyo husababisha prosesa kufanya kazi sana na kupelekea simu kupata Joto.
FANYA HAYA ILI KUEPUKANA NA SIMU KUPATA JOTO
  • Weka au Tumia Smartphone Yako Katika Mazingira yenye Mzunguko Mzuri wa Hewa.
  • Funga Apps Ambazo huzitumii kwa Muda Huo na Unstall Apps ambazo Huzitumii kabisa.
  • Ondoa Kava Pindi Simu Ipatapo Joto kali Ili kuruhusu Simu kupoa.
  • Zima simu yako na Iache Ipumzike Angalau kwa dakika chache.
  • Tumia ‘Earphones’ kuongelea Pindi uwapo na maongezi marefu.
  • Hakikisha Betri Na Chaja Unayotumia ni sahihi na Orijino kwa ajili ya Smartphone yako.
  • Tatizo likiendelea kuwepo baada ya kufanya yote hayo, Tafadhali peleka simu yako kwa fundi kwa Msaada Zaidi
EPUKA KUFANYA HAYA PINDI SIMU IPATAPO MOTO
Usiweke smartphone yako Kwenye Jokofu au Kiyoyozi Ili kuipooza haraka, Kufanya hivyo kunaweza kuaribu kabisa simu yako.

from Blogger http://ift.tt/2m0Myzd
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2lee7DC

No comments:

Post a Comment