Tuesday 2 May 2017

TzTown Tv: ALIZETI SISIUZWE BILA KUPITISHWA KIWANDANI, ‘MWENGE WAZIMULIKA’

WAKAZI wilayani Wanging’ombe Mkoani Njombe wametakiwa kujikita kwenye kilimo cha alizeti na kuanzisha viwanda vidogo vidogo ama kupileka kiwandani malighafi hizo na kuuza Bidhaa zitokanazo na Alizeti kwa tija.
Kauli hiyo inatolewa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Amour Hamad Amour wakati Mwenge huo ukiwa katika halmashauri hiyo na kuangazia miradi mbalimbali iliyo jengwa na wananchi na ile iliyo jengwa na serikali.
Mwenge wa Uhuru unakuwa kwa siku moja katika halmashauri ya wilaya ya Wangingombe na kuangazia miradi mbalimbali, katika miradi hii kiongozi wa Mbio hizo anatoa shime kwa wakulima wa Alizeti.
Pamoja na kutoa kauli hiyo Mwenge wa Uhuru unaangazia pia miradi ya Ufugaji wa Ngombe, Nyuki, pamoja na kufungua kituo cha afya pia uzinduzi wa kiwanda cha utengenezaji wa Viungo bandia vya Binadamu.
Mwenge wa Uhuru pia unazindua daraja ambalo ni kiungo cha wakazi wa Ilembula na Wangingombe ambapo kiongozi wa Mbio Hizo analidhishwa na Ujenzi wa Draraja hilo.

from Blogger http://ift.tt/2oT2mWC
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2p10YMW

No comments:

Post a Comment