Friday 28 April 2017

DC MBEYA AAGIZA VYANZO VYAMAJI KUWEKEWA BIKONS

Mkuu wa
wilaya ya mbeya Wiliam Ntimika amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo
Americhior Kwilizira kuweka alama za bikoni katika vyanzo vyote vya maji ili
kuendelea kukabiliana na uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji unaoendelea
kufanyika na baadhi ya wananchi wasiotaka kutii sheria.
Ameyasema
hayo baada ya kupokea taarifa kutoka kikisi kazi maalumu kilichoundwa na makamu
wa raisi samia suluu hasani kwaajili ya kulinda hifadhi ya mto ruaha mkuu
ambapo ameiagiza kamati ya ulinzi kumkata mwananchi wa kijiji cha itala
jacksoni mwangupili aliyevamia chanzo cha maji katika bonde la paboyo na
kuufanya shuguli za kilimo pamoja kupanda miti isiyo rafiki na maji.
Mkuu huyo wa
wilaya pia amemwagiza mkurugenzi kuwaandikia barua uongozi wa reli ya uhuru
tazara kufuatia kuzua mamlaka ya bonde la mto mkoji kufanya uhifadhi wa chanzo
cha mto ilonjero kilichopo katika kijiji cha mwakwenje kata ya inyara ili
wakutane na kufanya mazungumzo ya pamoja.
Awali mwenyekiti
wa kikosi malumu ambaye katibu tawala wa mkoa wa Njombe JACKSONI SAITABAU
amemueleza mkuu hutyo wa wilaya kuwa kikosi kazi kimebaini uwepo wa wananchi
wananovamia vyanzo vya maji na kukimbia katika vyombo vya sheria ikiwemo mahaka
na takukuru  na kupata Baraka za
kuendelea kuharibu vyanzo vya maji.
Makamu wa
raisi samia suluu hasani akiwa mkoani iringa aliunda kikosi kazi wajumbe 14
ambao wananfuatilia na kubaini sababu zinazosababisha mto ruaha mkuu kushindwa
kutiririsha maji kwa mawaka mzima kama ilivyo kuwa awali ambapo sebabu moja
wapo ni inayochangia uharibifi wa vyanzo  vya maji  katika mikoa ya njombe na mbeya.

from Blogger http://ift.tt/2oDR9cC
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2qlKrEn

No comments:

Post a Comment