Tuesday 2 May 2017

tzTown Tv: Mwenge 2017 wazindua miradi 8 Makete

WAZAZI na walezi hapa nchini wametakiwa kuwa karibu na watoto wao na kufuatilia nyendo zao ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza ili kupambana na madawa ya kulevya huku tabia za kutumia madawa ya kulevya zikidaiwa kuanza kutokana na ushawishi wanao upata watoto kutoka katika makundi na kuingi katika matumizi ya dawa za kulevya.
Hamasa hiyo inatolewa na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa wakati akifungua klabu ya wapinga madawa ya kulevya katika shule ya sekondari Matamba Wilayani Makente Mkoani Njombe ambako Mwenge huo umeangazia Miradi nane ya maendeleo, ya kujamii, na afya.
Wanafunzi watatoa ahadi ya kupambana na madawa yakulevya katika maeneo yao na kutoa elimu kwa wenzao, pia klabu ya wapingarushwa nayo ikifunguliwa kwaajili ya kutoa elimu kwa wanafunzi na jamii.
Bangi inateketezwa kuashilia kupambana na madawa ya kulevya huku kiongozi huyo akimpata mkuu wa wilaya kuendelea kuteketeza mashamba ya Bangi wilayani humo.
Mwenge wa Uhuru pia unaweka jiwe la msingi katika ujenzi wa chumba cha kuhifadhi Matunda ambacho kitakuwa kukipokea matunda kutoka maeneo mbalimbali na wanunuzi kufuata hapo.

from Blogger http://ift.tt/2qzEt2L
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2qzRhq2

No comments:

Post a Comment