Wednesday 12 August 2015

Kilicho sababisha Makete Uchaguzi kura za maoni urudiwe hiki hapa


CHAMA Cha Mapinduzi CCM wilaya ya makete Mkoani Njombe
ambacho Kesho kinarudia uchaguzi wake wa kura za maoni, kimejipanga kwa kuweka
wasimamizi watatu katika kila kituo cha uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha kuwa
mapungufu yaliyo jitokeza kuto jitokeza tena.
Akizungumza na Elimtaa Mkoani Njombe kwa njia ya simu katibu
wa chama hicho wilaya ya Makete Salum Chone  alisema kuwa chama hicho kimejipanga
kuhakikisha kuwa makosa yaliyo jitokeza katika kura za maoni hayajitokezi mapema.
Alisema kuwa chama hicho kwa wilaya ya Makete kulitokea
makosa ya wagombea kutangaza matokeo kabla ya kutangazwa na Mkurugenzi wa
uchaguzi wa wilaya hiyo.
Alisema kuwa kueopusha matokeo yatakayo sababisha malalamiko
ni kuhakikisha kuwa kila kituo cha uchaguzi kunakuwa na wasimamizi watatu.
Choneuchaguzi uliopita kulikuwa na shida ya wasimamizi kuto
kuwa na maadili na kutoa matokeo ya wagombea kabla ya kufika kwa Mkurugenzi wa
uchaguzi.
“Katika uchaguzi uliopita kulikuwa na malalamiko kutoka kwa
wagombea kuwa matokeo yalitolewa kabla ya Mkurugenzi wa uchaguzi ndio
malalamiko makubwa yaliyo sababisha matokeo kupingwa katika jimbo hili,”
alisema Chone
Alisema kuwa kuna baadhi ya wagombea walishiriki kubadilisha
matokeo kwa kushirikiana na mawakala wa uchaguzi na kusababisha wengine
kulalamika kutokana na kuto kuw ana imani na baadhi ya mawakala wa uchaguzi.
“Kuna baadhi ya wagombea walishirikiana na mawakala
kubadilisha matokeo ya uchaguzi na kitu hichi pia kilisababisha kutokea kwa
malalamiko,” Chone
Kwa upandewake katibu wa CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpagike
alisema kuwa anaelekea huko na siku ya Kesho wakati uchaguzi unaendelea akakuwa
wilayani Makete kwaajili ya uchaguzi huo.

Matokeo ya awali katika uchaguzi wa kwanza jimbo hilo kulikuwa na wagombea watano walliokuwa waking’ang’a kuchaguliwa na wananchi kuwakilicha chama chao katika uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu mbunge wa jimbo hilo Binilith Mahenge alipata kura 8534 Norman Sigala kura 8211, Bonic Muhami 500, Fabianus Mkingwa kura 466 na Lufunyo Rafael 226.




from Blogger http://ift.tt/1TtPgmj

via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/1hygTyQ

No comments:

Post a Comment