Wednesday 12 August 2015

AMA KWELI! AKUFUKUZAYE HAKWAMBII TOKA….

Gazeti la Marca limeripoti kwamba, Manchester United wamejumuisha jina la golikipa wao, David De Gea katika kikosi watakachotumia kwenye michuano ya Uefa Champions League msimu huu.
Hii ni taarifa mbaya kwa klabu ya Real Madrid ambayo wanaiwinda saini ya nyota huyo wa kimataifa wa Hispania.
De Gea mwenye umri wa miaka 24 aliyeomba kutimkia Santiago Bernabeu,  uhamisho wake umezungumzwa sana majira haya ya kiangazi, lakini sasa ripoti mpya kutoka Old Trafford inasema kwamba, kocha Louis van Gaal ameiambia Real Madrid kwamba, kama inataka kumsajili inatakiwa kulipa dau litakalovunja rekodi ya dunia la paundi milioni 32 .
Agosti 18 mwaka huu, Mashetani wekundu watacheza mechi ya kwanza ya raundi ya mwisho ya mtoano dhidi ya Club Brugge ya Ubelgiji na wanatarajia kutuma jina la De Gea makao makuu ya UEFA kwa ajili ya kucheza Champions League, wakimaanisha Mhispania huyo haendi popote.
Mpaka kufikia Jumatatu, United wanatakiwa kuongeza mchezaji mmoja katika kikosi chao cha Uefa na itawafurahisha mashabiki wa klabu hiyo kama Van Gaal atasajili mchezaji mpya ili ajumuishwe.
Wakati huu dirisha la majira ya kiangazi likielekea kufungwa Septemba mosi mwaka huu, United wamekuwa wakihusishwa kumsajili winga wa Barcelona, Pedro Rodriguez na winga wa Benfica, Nicolas Gaitan.




from Blogger http://ift.tt/1Tu0Pde

via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/1hygTPl

No comments:

Post a Comment