Thursday 20 August 2015

ZEC yaanza kutoa Fomu za wagombea Urais, wajumbe wa BLW na madiwani


Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imeanza utaratibu wa kutoa fomu za uteuzi wa wagombea kwa nafasi za Urais,Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani walioteuliwa kihalali katika vyama vyao. Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.  
Mh.Jecha Salim Jecha leo tarehe 17.08.2015 kwa nyakati tofauti amekabidhi fomu hizo kwa mgombea wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya TADEA Bw. Juma Ali Khatibu na Mgombea wa Urais wa Chama cha AFP Bw. Said Soud Said katika hafla iliyofanyika huko hoteli ya Bwawani.
Akizungumza kabla ya kuwakabidhi fomu hizo Mh.Jecha amewasisitiza wagombea hao kufuata utaratibu maalum uliowekwa wa ujazaji wa fomu hizo na kuandika taarifa zao kwa usahihi ili kuiondoshea usumbufu Tume wakati wa kufanya kazi zake. Amefahamisha kuwa kila Mgombea kwa tiketi ya urais atalazimika kutafuta wadhamini wasipungua mia mbili (200) kwa kila mkoa na kulipia kiasi cha shilingi milioni mbili wakati wa kuzirejesha fomu hizo.
Aidha wagombea hao wamesema lengo lao ni kudumisha amani iliyokuwepo na kuhakikisha kila mwananchi anapata maisha bora.
Nae Afisa uandikishaji Wilaya ya Magharibi Nd. Ali Rashid Suluhu leo amekabidhi fomu za uteuzi wa wagombea wa nafasi za Uwakilishi na Udiwani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Magharibi A na B huko ofisini kwake Maisara Mjini Zanzibar. Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inaendelea kukabidhi fomu za uteuzi kwa wagombea wa nafasi mbali mbali wa vyama vya siasa nchini ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.


from Blogger http://ift.tt/1MGkubp
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/1NHOCjJ

No comments:

Post a Comment