SERIKALI imesema kuwa uhakiki wa watu wanao nufaika na mradi wa Tasaf awamu ya tatu Wa kunusuru kaya masikini uendelee kwa umakini ili wanao stahili pekee kubaki na jamii nayo kutakiwa kufichua wale ambao wanaona hawastahili kupata fedha hizo.
Katika mkoa wa Njombe taarifa zinasema kunawatu wamebainika kuwa hawana sifa na wameondolewa katika mpango huo ili kupisha wale ambao wanastahili kupata Pesa hizo kwaajili ya kunusuru kaya maskini.
Kauli hiyo inatolewa wakati kamati ya bunge ya kudumu ya Utawala na Serikali za mitaa ikiwa mkoani Njombe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe Agela Kairuki baada kupokea taarifa ya kutekeleza miradi mbalimbali ya Tasaf mkoani humo.
Akitoa taarifa ya mkoa wa Njombe Katibu tawala wa mkoa wa humo amesema kuwa uhakiki unaendelea kila kijiji na mtaa mkoani humo kubaini wasio na sifa.
Wanufaika wanatoa shuhuda zao jinsi walivyo nufaika wakati kamati ilipo watembelea katika kijiji cha Uwemba walipokutwa wakiendelea kupokea fedha zao.
Naye Kaimu mwenyekiti wa kamati hiyo anasema kuwa wanafaika hao wajiadhari na kuuza maeneo yao kwa kuwa maeneo hayarudi yakiuzwa na kuwataka waendelee kujiandaa kwa kufungua miadi ya kujiongezea kipato.
Tazama video hapa chini Wanufaika wa tasafu wato machizi…………..
from Blogger http://ift.tt/2oojjIb
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2ns3lrg
No comments:
Post a Comment