Sunday, 19 February 2017

Trump avishambulia vyombo vya Habari

Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine tena amevishambulia vyombo vya habari katika “mkutano wa kisiasa nchini Marekani” tukio hilo lilifanyika katika jimbo la Florida.
Aliuambia umati mjini Melbourne kwamba vyombo vya habari havitaki kabisa “kusema ukweli” na kwamba waandishi wa habari wana ajenda zao fiche.
Pia Trump ametetea mafanikio ya utawala wake, akisisitiza kuwa sasa yeye ni “kinara wa roho ya matumaini inayokwenda kwa kasi kote Marekani”, huku akirejelea ahadi nyingi alizotoa wakati wa kampeni yake kuhusiana na ufufuaji wa uchumi na uimarishaji wa usalama.
Rais Donald Trump leo Jumapili atawahoji watu ambao watasimamia nyadhifa nne za washauri wa kitaifa wa maswala ya usalama.
Watu hao wanamjumuisha Keith Kellogg — kaimu mshauri mkuu wa usalama wa kitaifa, baada ya kutimuliwa kwa Michael Flynn juma lililopita na Balozi wa zamani wa Marekani katika umoja wa mataifa John Bolton.
Shabiki wa Trump katika mkutano wa kisiasa huko Florida. Picha 18 Februari 2017
Majemedari wengine wawili ni H.R McMaster na Robert Caslen, pia wamo katika orodha hiyo.
Msemaji wa White House Sean Spicer, amesema kuwa jenerali mstaafu na kinara mkuu wa zamani wa shirika la ujasusi nchini Marekani CIA David Petraeus, si miongoni wa watakaohojiwa.
Michael Flynn alijiuzulu Jumatatu ya juma lililopita, kutokana na utata kuhusiana na vikwazo vya Marekani kwa Moscow uliomzingira baada ya kukutana na balozi wa Urusi jijini Washington.
Waandamanaji wameapa kujipanga pembezoni mwa njia kuelekea atakakokuwa akifanyia mahojiano hayo.
Siku ya Jumamosi, Rais Trump na mkewe Melania walisalimiwa na maelfu ya wafuasi wao kwenye mkutano huo kwenye jimbo ambalo alipata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu mwezi Novemba 2016.

from Blogger http://ift.tt/2lZXXfJ
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2lj38Y1

No comments:

Post a Comment