Mjini Johannesburg, mvulana wa miaka 10 alilazimishwa kulala kifudifudi wakati mama yake akibakwa kwa muda wa saa nne katika teksi, hii ni kwa mujibu wa ripoti kutoka Afrika kusini.
Mvulana huyo na mama yake wanadaiwa kulaghaiwa kuingia ndani ya gari dogo la abiria (teksi). Baada ya mama na mwanae kuingia ndani ya teksi, mvulana alilazimishwa kulala kifudifudi chini kwenye sakafu ya gari hilo, huku wanaume watatu wakimbaka mama yake. Kabla ya kufanyiwa vitendo hivyo mama aliamrishwa kukabidhi kadi yake ya benki pamoja na namba za siri (PIN) za kadi hiyo, na wanaume hao waliokuwa na bunduki.
Inadhaniwa kuwa kuwa hili lilikuwa ni shambulio la hivi karibuni la genge la majambazi.
Taarifa za kwanza za watu wanaotumia magari kufanya matukio ya ubakaji ziliripotiwa mwaka mmoja uliopita. Kwa mujibu wa rekodi za Roodeport, matukio ya awali ya ubakaji yaliripotiwa mwezi Machi 2016, huku matukio mengine matatu yakifanyika katika kipindi cha wiki ya mwisho ya mwezi Juni. Matukio yote yalifanyika katika eneo la Soweto mjini Johannesburg.
Hata hivyo haijabainika wazi kuwa ni mashambulio mangapi yaliyokwisha kutokea huko katika kipindi cha miezi 12 bila kuripotiwa, na kama yote yalitekelezwa na kundi hilo hilo.
Luteni Kanali Lungelo Dlamini amesema “Kikundi cha wanaume watatu ama wawili waliokuwa wakiendesha magari mawili tofauti ya [Toyota] Quantums, moja la rangi ya kijivu na jingine la rangi nyeupe, yaliwachukua wanawake wawili yakijifanya ni magari ya teksi, wakawapora kwa silaha na baadae kuwabaka.”
Bwana Dlamini amesema kuwa haijabainika wazi kuwa magari hayo ya Quantum yalikuwa yana njama moja ama kila moja lilikuwa linatekeleza uhalifu huo kivyake.
Hadi sasa, wanawake wawili , akiwemo mama wa mvulana huyo , wamekwisha zungumza na vyombo vya habari vya Afrika Kusini, kuelezea kilicho wasibu.
Muathiriwa huyo aliliambia shirika la habari la EyeWitness News kwamba alikuwa anaomba wakati wa tukio hilo wabakaji hao wasimuumize mwanae.
Afrika Kusini ni nchi iliyoripotiwa kuwa na matukio mengi zaidi ya ubakaji duniani.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA
from Blogger http://ift.tt/2nT5ssZ
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2nyvG39
No comments:
Post a Comment