Mhagama alisema huenda idadi hiyo ikaongezeka kutokana na kuendelea kuwasili kwa wananchi hao.
Wakati Mhagama akieleza idadi ya Watanzania waliorudishwa nchini, mwanamke mmoja aliyekuwa akitokea nchini Msumbiji amefariki dunia usiku wa kuamkia juzi katika Hospitali ya Rufaa Ligula mkoani Mtwara alikokuwa akipatiwa matibabu.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, George Salala alisema mwanamke huyo ametambuliwa kuwa ni Jackline Gryson (26) mkazi wa mkoani Iringa.
Alisema alipokewa katika kivuko cha mpaka wa Kilambo hali yake ikiwa mbaya kutokana na ugonjwa.
Wakati huohuo; Kaimu kamanda huyo alisema Mkoa wa Mtwara unaendelea kuwapokea Watanzania wanaorudishwa nchini kutokea Msumbiji wanakodaiwa kuishi kinyume cha sheria.
from Blogger http://ift.tt/2lGKV9q
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2m76Eox
No comments:
Post a Comment