Moja ya magazeti ya jana yalichapisha habari inayomtaja mbunge huyo kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya ambayo imekuwa ikipigwa vita kila kona ya nchi kutokana na kupoteza nguvu kazi ya taifa
Gazeti hilo limeandika kuwa jina la Ridhiwani limetajwa katika orodha ya watuhumiwa wa dawa za kulevya na kuwa uchunguzi utafanyika. Pia limesema mbunge huyo ametoa kauli nzito kwa hadhara
Kiongozi huyo kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa,’hafanyi biashara hiyo haramu wala hakuwahi kufikiria kuifanya na kwamba nafsi yake i tayari kufa masikini kuliko kupata utajiri kupitia njia hiyo
Aidha, ameeleza kuwa anaamini kwamba uchunguzi utafanywa ili kuweza kuweka mambo sawa kwani yeye hana kitu chochote cha kuficha. Amesema kwamba, maneno hayo ya shutuma juu yake ni uongo na kwamba yametolewa na watu wasiomtakia mema na wasio na haya.
from Blogger http://ift.tt/2mkDIZu
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2l6R4Ip
No comments:
Post a Comment