Wednesday, 22 February 2017

Paul Makonda Kujibu Tuhuma Zilizoelekezwa Kwake Kupitia PB ya Clouds FM Kesho Februari 23, 2017

Wadau, amani iwe kwenu.

Kwa siku kadhaa, kumekuwa na tuhuma zinazoelekezwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, PAUL MAKONDA. Tuhuma hizo zimeanza kutolewa mara baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kuasisi mapambano dhidi ya madawa ya kulevya ambayo yameshika kasi sasa baada ya Rais MAGUFULI kumteua ROGERS SIANGA kuwa kamishna Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini. Miongoni mwa tuhuma hizo ni pamoja na;

1. Kutumia Jina lisilo lake la PAUL CHRISTIAN ambapo mwenye jina hilo ni Mtangazaji wa Radio huko Tabora. Kwa mujibu wa tuhuma hizo, PAUL MAKONDA majina yake halisi ni DAUDI ALBERT BASHITE. Jina la PAUL CHRISTIAN lilikuja baada ya MAKONDA kutumia cheti cha mwenzake ili aingie Jeshi la Polisi kwa vile yeye alifeli mtihani wa kidato cha nne. Kwa vile PAUL CHRISTIAN halisi alifaulu division One, Busweru Sekondari na kupangiwa Tabora Boys ambako alishindwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano kwa kukosa ada, MAKONDA akatumia cheti hicho kujiendeleza kitaaluma. Tuhuma hizi zimezushwa na MANGE KIMAMBI ambaye mpaka sasa ameshindwa kuweka ushahidi wa hoja zake.

2. Kununuliwa na wauza madawa ya kulevya gari la kifahari aina ya LEXUS lenye thamani ya zaidi ya milioni 400…..Tuhuma ya Bungeni

3. Kumnunulia mke wake gari ya kifahari aina ya Benz lenye thamani ya zaidi ya milioni 500 na kumkabidhi wakati wa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa…Tuhuma ya Bungeni

4. Kununua Appartment Viva Tower, Dar es Salaam….Tuhuma ya Bungeni

6. Kujenga jengo la ghorofa huko Mwanza ambalo limekamilika ndani ya mwaka mmoja. Hata hivyo watoa tuhuma hizi waliingia mkenge baada ya kuweka picha ya jengo ambalo ni Hotel iliyopo Kigoma.

7. Kusafiri kwenda Marekani na Ufaransa na kukaa siku 21 huku akipanda ndege Daraja la Kwanza ambapo gharama ya nauli kwa yeye na mkewe ni Dola za Kimarekani 14,000 kwenda pekee. Kwamba, kwa mshahara wa Mkuu wa Mkoa, usingetosha kugharamia safari hiyo…..Tuhuma ya Bungeni

8. Kumpangishia nyumba ya kifahari AGNES MASOGANGE eneo la Makongo, Dar es Salaam kwa vile ni mpenzi wake na ndio maana hakumtaja kwenye orodha ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya……Tuhuma ya Wema Sepetu.

9. Kukarabati jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam bila kufuata taratibu za manunuzi kwa gharama ya Milioni 400…..Tuhuma ya Bungeni

10. Kumpigia simu Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya na kumtishia kuwa yeye pamoja na wabunge wengine kama PETER MSIGWA, JOSEPH MBILINYI aka SUGU, HALIMA MADEE, JOSEPH KASHEKU aka MSUKUMA atawashughulikia na kwamba wabunge hao si lolote, si chochote…..Tuhuma za Bungeni.

11. Tuhuma ya kumporomoshe matusi Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Jambo Leo baada ya kumuuliza swali kuhusu tuhuma za kutumia cheti kisicho chake cha kidato cha nne………Tuhuma ya Jambo Leo

Tuhuma ni nyingi na naamini wadau mtaongezea na mimi nitaedit uzi huu ili kuleta mtiririko sawia. Hata hivyo, pamoja na shutuma hizo kuporomoshwa juu yake, PAUL MAKONDA aliamua kutumia busara ya kukaa kimya ili kuepusha mijadala isiyohitajika na hivyo kumtoa kwenye harakati za kupambana na madawa ya kulevya.

Akiongea kwenye kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa hewani na Clouds FM Radio, Mtangazaji wa kipindi hicho, BARBARA HASSAN ametoa taarifa kuwa amempigia simu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam PAUL MAKONDA na kumuomba ajitokeze kupitia kipindi hicho na kujibu tuhuma dhidi yake. Habari njema ni kwamba, PAUL MAKONDA amekubali wito huo na kwamba kesho tarehe 23 Februari 2017 atakuwa hewani ‘LIVE’ kuanzia saa 12.30 Asubuhi kupitia KAKAKUONA na kuendelea hadi mwisho wa kipindi cha POWER BREAKFAST cha Clouds FM Radio.

By Lizaboni/Jamii Forums

from Blogger http://ift.tt/2mbsxmo
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2lnyVZI

No comments:

Post a Comment