Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Unicef Dkt Jama Gulaid akitoa hotuba katika sherehe ya makabidhiano ya magari ya kubebea wagonjwa Mkoa wa Mbeya15 Octobar 2015 |
Mwakilishi UNICEF Dkt Jama Gulaid kulia akimkabidhi Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Ndugu Kastro Msigala taarifa muhimu za magari hayo yenye thamani ya shilingi mil 700 . |
Timu ya Uendeshaji wa huduma za za Afya Mkoa wa Mbeya |
Meza kuu katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Mbeya na wawakilishi wa Shirika la UNICEF. |
Meza kuu katika picha ya pamoja na waganga wakuu wa Halmashauri za Mkoa wa mbeya . |
Meza Kuu katika picha ya Pamoja na timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya Mkoa wa Mbeya . |
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi shirika la UNICEF. |
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linalo shughulikia watoto Duniani (UNICEF) limekabidhi msaada wa magari kumi ya Kubebea wagonjwa yenye tahamni ya shilingi mil 700.7 kwa serikali ya Mkoa wa Mbeya .
Aidha shirika hilo lina mpango wa kuboresha vituo 184 vya kutolea huduma za afya katika mkoa huo wa mbeya ambavyo ni vituo afya na hospital 30 pamoja na zahanati 154 sanjali na kuvipatia vifaa muhimu vya kutolea mafunzo kwa watumishi wake.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Octobar 15 mwaka huu Mwakilishi wa shirika la UNICEF nchini Tanzania Dkt Jama Gulaid amesema shirika hilo limetenga kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa ajili ya mradi huo.
Amesema mchango wa UNICEF katika sekta afya na lishe hapa mkoani mbeya imepanua wigo kutoka halmashauri mbili za mkoa huo hadi kufikia halmashauri zote katika kipindi cha miaka miwili .
Aidha Dtk, Jama amesema katika kukabiliana na magonjwa na vifo vya watoto na wanawake wajawazito ,UNICEF imechangia vifaa tiba muhimu ikiwa ni pamoja vile vya uchunguzi wa ujauzito ,upasuaji sanjali na vifaa kuwasaidia watoto wachanga kupumua mara wanapo zaliwa na vifaa vingine vya utoaji wa huduma katika idara ya uangalizi maalumu ICU.
Aidha amewataka viongozi hao wa mkoa wa Mbeya kuhakikisha wanaweka juhudi kubwa zaidi katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga kwa kuhakikisha kwamaba kina mama wajawazito wote wanapata huduma za afya bure kwa wakati.
Awali akisoma taarifa ya huduma za afya ya uzazi na mtoto katika mkoa mbeya mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto Ndugu Prisca Butuyuyu amesema toka shirika hilo la UNICEF lianze kufanya mwaka 2012 huduma za afya zimeimalika kwa kiasi kikubwa hususani kwa kuweza kuzuia vifo vya uzazi na vya watoto wachanga.
Amesema kwa ujumla hali ya vifo hususani vilivyokuwa vinatokea katika vituo vya huduma vimepungua kutoka 140 kwa mwaka 2012 na kufikia vifo 94 kwa kwa mwaka 2014 pamoja na kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka 602 kwa mwaka 2012 hadi kufikia 568 mwaka 2014 ambapo punguzo hilo ni sawa na asilimia 33.9 na 5.7 kwa watoto wachanga.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Kaimu katibu Tawala Ndugu Kastro Msigala amelishukuru shirika hilo kwa msaada wa magari hayo sanjali na kutoa wito kwa viongozi wa halmashauri ambao ni wakurugenzi na waganga wakuu kuhakikisha wanayatunza magari hayo ili yaweze kutoa huduma stahiki kwa wananchi.
Msaada huo wa magari imegawanywa katika halmashauri zote mkoa huo wa mbeya ambazo ni Ileje,Mbozi,Mbeya vijijini,Rungwe,Busokelo,Mbarali pamoja na Kyela na Momba .
Mwisho
(Imeandaliwa na Jamiimojablog Kanda ya Nyanda za juu kusini Mbeya 0759406070 )
from Blogger http://ift.tt/1MtioGG
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/1Mtjd2e
No comments:
Post a Comment