Wednesday 14 October 2015

Mgombea Ubunge ACT Wazalendo anusulika kupigwa na watu anaodai ni CCM



MGOMBEA wa ACT-Wazalendo jimbo la Njombe Kusini, Emilian Msigwa amenusulika kupigwa na watu wanao daiwa ni wafuasi wa chama cha mapinduzi akiwa katika mkunano wa kampeni za uchaguzi huku mfuasi mmoja wa chama hicho kukimbizwa Hospitalini.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe Mgombea
huyo alilalamika kuhusiana na vurugu hizo Juzi akisema kuwa zilitokea juzi
katika mkutano wake uliokuwa ukifanyika katika kijiji cha Yakobi cha jimbo hilo
mkoani Njombe.
Msigwa alisema kuwa katika kata ya yakobi amekuwa akipata
shida ya kufanya kampeni katika vijiji vyake kutokana mgombea udiwani wa kata
hiyo kupitia CCM kuweka vikwazo vya kuzuia mikutano ya chama hicho kwa kuweka
naye ratiba zake na kufanya hujima na watendaji wa vijiji hivyo.
Alisema kuwa mgombea wa udiwani awali wlitakiwa kufanya
mkutano katika kijiji hicho alicho letewa vurugu lakini alizuia gari ya
matangazo na kusema kuwa katika kijiji hicho kuna kampeni za CCM kwa mujibu wa
ratiba.
Alisema kuwa baada ya kufikishana katika Ofisi za kijiji cha
Yakobi alibadilishiwa ratiba na kuwa mgombea huyo alikuwa  na ratiba ya siku nzima katika kijiji hicho
hivyo siku ya Juzi baada ya kupangiwa ratiba kwa siku hiyo akiwa katikati ya
mkutano aliona gari ya iliyo na bendela za CCM iliingia katika mkutano wake.
Akielezea mkasa huo alisema kuwa baada ya gali hiyo kuingia
katika mkutano wake ilisimama kati kati ya jukwaa lake na upande walio simama
wananchi na kuwa baada ya hapo uliwashwa muziki wa CCM na baada ya muda kuna
watu walio na miili mikubwa (Mabaunsa) walishuka katika gali na kumfuata mfuasi
wa chama hicho ambaye ni maarufu aliye toka chama cha Demokrasia na maendeleo
Chadema.
Alisema kuwa mfuasi hiyo Ally Mhagama maarufu Sagasaga
alivamiwa na watu hao na kuanza kupigwa kasha kupelekwa katika gari ya CCM
wakitaka kuondoka nae Wananchi wa liokuwepo kwenye mkutano hawakukubari
waliamua kuaza kupambana nao.
Alisema wakati vurugu hizo zinatokea Polisi wa kulina
uvunjifu wa amani katika mkutano wake hawakuwepo na kuwa yeye alikimbilia kweye
gali akiwa anajiokoa.
Alisema kuwa wakati vurugu zinaendelea Mgombea Udiwani kata
ya Yakobi alionekana eneo la tukio akiwa ameshika mawe mawaili akitaka
kuwarushiwa wananchi na baada ya muda polisi walifika eneo la tukio.
Akizungumzia ulizi wa polisi katika mikutano yao alisema
kuwa katika mikutano yao mingi ya vijiji huwa wanaenda bila ya kuwa na polisi
kutokana na umbali wa maeneo na kuwa na imani ya kuwa na amani katika maeneo
hayo na kusema kuwa mikutano ya mjini huwa wanakuwa na Polisi.
“Katika mikutano yetu yote wanayo ya vijiji huwa tunafanya
bila ya kuwa na polisi kwa kuwa hawawezi kufika eneo la kampeni kutokan ana
ubali wa baadhi ya maeneo na kuwapo na amani katika vijiji vingi lakini kwa
maeneo ya mjini huwa tuna kuwa na askali na katika maeneo tunaona viashiria vya
ukosefu wa amani huwa tuna waambia polisi wanakuwepo,” alisema Msigwa.

Msigwa aliongeza kuwa ameshiriki chaguzi nyingi lakini hajawahi kuona CCM wanafanya vurugu lakini vyama vingine lakini vyama vingine ni kawaida lakini mwaka huu ni tofauti na kuwa CCM wamebanwa.

“Chama cha mapinduzi mwaka huu kimebanwa na kinatumia mbinu mbalimbali kama zilivyonifanyia mimi mwaka huu,” aliongeza Msigwa.

Akizungumza
na Nipashe kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, Wallboard Mtafungwa,   kwa
njia ya simu alisema kuwa tukio hilo limewafikia na kuwa wanalifanyia uchunguzi
huku akisema kuwa katika mkutano huo kulikuwepo na askari ambao haikuwa rahisi
kufahamika.
Aliongeza kuwa
jeshi hilo bado halijajua ni wakinanani wahusina kwa kuwa baada ya tukio
walitokomea kusiko julikana.


from Blogger http://ift.tt/1NGyG4Z
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/1X2ImIs

No comments:

Post a Comment