Tuesday, 8 September 2015

Lowassa: Sina muda wa kujibu matusi ya CCM 


Mgombea urais wa Tanzania anayewakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa
akiwasili kwenye mkutano wa Mbezi, Jimbo la Kibamba
MGOMBEA urais wa Tanzania anayewakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa
amesema hana muda wa kujibu matusi na kejeli zinazotolewa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
dhidi yake.

 Badala yake amesema anatumia muda uliobaki wa kampeni kutafuta kura kwa wananchi kwa kunadi ilani
ya chama chake.

Anaandika Pendo Omary
Kauli hiyo ameitoa kama mrejesho wa kampeni ya kimkakati inayofanywa na makada wa CCM walioamua
kumshambulia wakimtuhumu kuwa hafai urais, ni kapi, fisadi na mgonjwa.
“Sina muda wa kuwajibu. Tukutane kwenye sanduku la kura. Katika siku 48 zijazo, mtaamua juu ya ajira za
vijana, afya kama mtaendelea kulala watano watano, mtaamua juu ya elimu yenu ambayo mimi natamani
iwe bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu, maslahi ya walimu na viwanda vyenye ajira,” amesema Lowassa
ambaye tangu alipoanza kampeni amekuwa akiieleza Ilani ya Uchaguzi iliyopitishwa na UKAWA.
Lowassa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumpigia kura Oktoba 25, na kuzilinda kura kwa
sababu tayari anazo taarifa kuwa CCM wamejipanga kuiba kura.
Lowassa alipanda jukwaani
Viongozi walianza kuhutubia saa 11:38 na kumaliza saa 12:10 jioni huku wananchi wakifika viwanjani hapo
kuanzia saa 4 asubuhi.
Kulitokea tafrani kidogo pale viongozi wasimamizi wa jukwaa walipoamua kuwaondoa askari tisa wa Jeshi
la Polisi waliofika mbele ya jukwaa kabla ya viongozi kwa nia ya kutoa ulinzi. Ilielezwa kuwa viongozi
waliona “polisi hawaaminiki.”
Aidha, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye aliyejiunga na Ukawa wiki mbili zilizopita, amesema CCM
hawataki kuachia madaraka licha ya kutokubalika kwa wananchi kwa sababu ya kudumaza maendeleo na
kukumbatia rushwa na kujikita kumshambulia yeye na Lowassa.
“Nasisitiza watatoka tu, wamebaki na kazi ya kumchafua mgombea wetu na mimi. Lowassa alitoka
serikalini miaka minane iliyopita, hata Rais Jakaya Kikwete alisema lililomkuta ni ajali ya kisiasa na
kwamba hakuhusika na Richmond. Kwa vile leo ametoka CCM anaonekana ni mbaya,” amesema Sumaye.
Akihutubia jukwaani, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameionya CCM na serikali kuacha
kuitumia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhujumu matokeo ya uchaguzi mkuu.
“CCM na serikali wanahofu. Baada ya kumchafua mgombea wetu pia wana mkakati wa kuitumia TRA
kuingiza bidhaa mfano mafuta bila kulipa ushuru ili kuyauza na kununulia shahada za kupigia kura,”
ametuhumu.
Mgombea ubunge wa jimbo la Kibamba, John Mnyika alitumia fursa hiyo kujinadi akisema Lowassa
atakapochaguliwa kuwa rais atahakikisha serikali inapeleka maji jimboni.
Mnyika ambaye alikuwa mbunge wa Ubungo, jimbo linalogombaniwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hali
Halisi Publishers Limited (HHPL), Saed Kubenea, alimtaja aliyekuwa Katibu Mkuu Chadema, Dk.
Willibrod Slaa kuwa sasa ni adui wa chama hicho.
Amesema Dk. Slaa baada ya kukaa kimya kwa zaidi ya mwezi, tangu Chadema kilipomkaribisha Lowassa
kujiunga, ameibuka na kusema chama kimepoteza misingi yake kwa kumpokea Lowassa na kumteua
kugombea urais, hatua inayoonekana ni ya makusudi ya kuinua CCM.
“Kuna watu wametoka chooni wameingizwa chumbani… na mwingine ametoka chumba cha Ukawa na
Chadema ameenda chooni. Tatizo la msingi adui yetu mkubwa ni CCM. Na sisi tunatangaza atakaeungana
na CCM pia ni adui yetu,” amesema Mnyika.
Kubenea amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 25 kumpigia kura Lowassa huku
wakikumbuka wanapaswa kuondoa maradhi makuu matatu yaliyotangazwa na Chama cha TANU
(Tanganyika African National Union) ambayo ni maradhi, umasikini na ujinga.
Lowassa aliyeteuliwa na Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) ameeleza hayo katika mkutano wa
kampeni kwenye viwanja vya Mbezi Mwisho, jimbo la

Kibamba, jijini Dar es Salaam.
9/8/2015 Lowassa: Sina muda wa kujibu matusi ya CCM | 2jiachie – Official Site
http://ift.tt/1KYhiGs 3/9
Share ! Tweet 0 Like 12 1
“Ili Lowassa aweze kufanya kazi vizuri akiwa rais, lazima tupeleke wabunge wengi wa Ukawa bungeni.
Twende tarehe 25 Oktoba kupiga kura huku tukikumbuka maneno ya rais mstaafu Benjamin Mkapa
aliyekaa madarakani kwa miaka 10 bila ya kutuondolea upumbavu na ulofa,” amesema Kubenea.
Mkapa alitoa maneno hayo jukwaani siku CCM ilipozindua kampeni yake kwenye viwanja vya Jangwani,
Dar es Salaam, alipolenga kumshambulia Sumaye, waziri wake mkuu wakati alipokuwa rais.
CHANZO: MWANAHALISI ONLINE

from Blogger http://ift.tt/1K3ohc1
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/1LgUZaO

No comments:

Post a Comment