Monday, 7 September 2015

Idara ya Uhamiaji ya Kenya yalaumiwa


Wakenya wanatumia njia za mkato kupata stakabadhi wanazohitaji, na hilo ni hatari kwa usalama wa taifa.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya Uhuru KenyattaKwa kipindi kirefu wakenya hasa wakaazi wa eneo la Pwani wamelalamikia kunyanyaswa na idara za usajili wa watu na ile ya uhamiaji  wakati wa kutoa vitambulisho vya kitaifa, vyeti vya kuzaliwa au hati za kusafiria.

Kutokana na malalamiko  hayo tume ya utekelezaji haki  imefanya uchunguzi na kutoa ripoti kuhusu chanzo cha matatizo hayo na kutishia  usalama wa taifa hilo.
Taarifa zinasema kwenye ripoti hiyo ni asilimia 2.8 ya wakenya wanaridhika  na huduma zinazotolewa na idara ya kutoa vitambulisho na uhamiaji , idara ambazo zinawafanya  wakenya kukosa stakabadhi halisi za kujitambulisha.
Naibu mwenyekiti wa tume hiyo Regina Muatha amesema kuwa hatua hiyo imesababisha wakenya kutumia njia za mkato kupata stakabadhi hizo suala ambalo ni hatari kwa usalama wa taifa.

from Blogger http://ift.tt/1NdvxYd
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/1QkdTC9

No comments:

Post a Comment