Saturday 11 February 2017

GWAJIMA ATOKEA POLISI JIONI HII

Ni kutoka kwenye headlines za sakata la dawa za kulevya kupitia kwenye orodha aliyoitaja Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenye awamu ya pili ambayo ilijumuisha majina ya watu 65 akiwemo Askofu Gwajima.
Kutoka Kituo cha Polisi Kati Dar es salaam jioni hii, camera ya AyoTV imemnasa Askofu huyo wa kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima akiwa anatoka kwenye kituo hicho cha Polisi alikokua ameshikiliwa toka Alhamisi kufuatia kutajwa kwenye orodha ya Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda.
Baadhi ya Waumini wa Kanisa lake walikua nje ya kituo hicho cha Polisi jioni hii na walisikika wakizungumza maneno mbalimbali ya kushukuru kama vile “Asante Yesu”
Video ya Tukio zima itakujia hapahapa TZTOWN KUTOKA MITANDAO RAFIKI

from Blogger http://ift.tt/2kwTCQ2
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2l5ihOK

No comments:

Post a Comment