Thursday 29 December 2016

TRUMP ALIKASHIFU BARAZA LA USALAMA LA UN

Rais mteule wa Marekani , Donald Trump, kwa mara nyengine tena amelikashifu shirika la Umoja wa Mataifa.
Kupitia akauntI yake ya Twitter, amesema shirika hilo linamsikitisha kwa madai kwamba badala ya kuwa shirika lenye hadhi kuu zaidi, limekuwa kama baraza la watu kukusanyika na kupiga gumzo.
Hii ni baada ya jaribio lake la kutaka kupinga azimio lililokemea mpango wa Israel kuendelea kujenga makaazi yao katika ardhi ya Wapalestina kufeli.
Trump alikashifu baraza la usalama la Umoja wa Mataifa
Trump
Baraza la usalama la Umoja wa Matifa limesema kuwa Israel inakiuka sheria za kimataifa kwa kujenga katika ardhi ya Wapelestina.
Azimiio hilo lilipitishwa Ijumaa iliyopita huku Trump akitoa onyo kwamba mambo yatakuwa tofauti wakati atakaposhika rasmi hatamu za uongozi wa Marekani.

from Blogger http://ift.tt/2iucDlx
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2hzr8rh

No comments:

Post a Comment