Wednesday 20 July 2016

RC. DR NCHIMBI: USAFI UWE NI TABIA NJOMBE

Mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi aliye vaa kofia ngumu mda mfupi baada ya kukabidhi pikipiki kwa washindi wa usafi kitaifa.



MKUU wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi amepinga wakazi wa
mkoa huo kufanya usafi wa mazingira wakati wa kampeni za usafi mazingira
kitaifa badara yake usafi kuwa ni tabia.

Dr. Nchimbi anawataka wakazi wa mkoa huo kujijengea tabia ya
kufanya usafi mara kwa mara kwenye mazingira yao.
Wito huo aliutoa juzi wakati akikabidhi zawadi kwa
halmashauri ya wilaya Njombe, Mji Njombe na vijiji vilivyo ongoza kitaifa mpaka
nafasi ya tatu vilivyotoka halmashauri ya wilaya ya Njombe.
Dr. Nchimbi aliwataka wakazi hao kutofanya usafi kwa mazoea
na kufanya usafi kama tabia ya wakazi wa Njombe na kusiwe na haja ya watu
kuwashindanisha.
Alisema kuwa haiwezekani watu wakawa wanafanya usafi mpaka
kuwe na mashindano kitu hicho ni cha hatari kwa kuwa wanaweza kuugua kama
hakuta kuwa na mashindano.
Mashindano hayo kitaifa ya usafi wa mazingira na ujenzi wa
vyoo bora mkoa wa Njombe umetwaa ushindi kwa halmashauri zake mbili za Njombe
Mji ambayo imepata Pikipiki ambayo imeongoza kwa halmashauri zote za miji
nchini.
Halmashauri ya wilaya ya Njombe ikiibuka mshindi kwa
halmashauri zote za wilaya nchini na kupata zawadi ya Pikipiki, na Gari moja
aina ya Landcruise Hadtop.
Hata hivyo vijiji hapa nchini ushindi uliangukia katika
vijiji vya halmashauri ya wilaya ya Njombe ambapo vijiji vitatu bora na kijiji
cha Wanginyi kikichukua nafasi ya kwanza kwa vijiji vyote Tanzania.
Emmanuel Mwenda ni Mwenyekiti wa kijiji cha Wanginyi mshindi
wa kwaza kitaifa anabainisha changamoto walizopitia kuupata ushindi huo.
“Katika mashindano haya tulikumbana na changamoto ya maji na
tatizo hili mpaka sasa lipo katika vijiji ninakotoka na vyoo vya masinki bila
kuwapo kwa maji usafi wake ni mgumu naomba serikali kutusaidia maji
yakapatikana” alisema Mwenda
Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri mbali na kuwapongeza
washindi kitaifa alisema changamoto ya maji kweye wilaya yake ishughurikiwe na
wakirugenzi ili wananchi wafanye shughuli zao na kuachana na mahangaiko ya
kutafuta maji.
 

from Blogger http://ift.tt/29SMycp
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2ab3YRZ

No comments:

Post a Comment