Monday 18 July 2016

ELIMU BURE WAALIMU WAOMBA MADARASA NA WAALIM KUONGEZWA

MIEZI sita baada ya sera ya elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka kidato cha nne hapa nchini waalimu wamebaini changamoto mbalimbali ambapo wanaomba serikali kuzishugulikia ili elimu bora itolewa kwa wanafunzi wengi walio jitokeza kupata elimu.
Baada ya sera hiyo kuanza wanafunzi wengi wamejitokeza kupata elimu, huku changamoto ya awali ya uchache wa madawati imetatuliwa tayari sasa wanafuzi wanakaa kwenye madawati lakini shida inakuja katika suala ya vyumba vya madarasa.
Waalimu mkoani Njombe pamoja na kumshukuru Rais wa jamuhuri ya Tanzania Dokta John Magufuli kuhakikisha kuwa wanafunzi wanakaa katika madawati wamemuomba Rais kutatua tatizo la uchache wa waalimu, vitendea kazi pamoja na madarasa kwa baadhi ya shule.
Victoria Kiwale, ni mwalimu wa wanafunzi viziwi kwenye shule wa watu hao mkoani Njombe anaomba serikali kuhakikisha kuwa watoto wanapatiwa wanafunzi wa kutosha hasa kuweka sawa uwiano kati ya wanafunzi na waalimu.
Tatizo hili linaenda sambana na uhutaji wa vitendea kazi kwa waalimu wanao fundisha watoto wenye uhitaji maalumu kama wale wenye uoni hafifu.
Mwalimu Subula Mligo anasema kuwa waalimu wanaofundisha watu wenye ulemavu wanauhaba wa vitu vya kufundishia hasa vile vya nukta nundu.
“Ombi langu kwa serikali ni kuwasaidia waalimu wenzangu kuwapatia vitendea kazi vya kufundishia tunashukuru sasa wanafunzi wanafundishwa wakiwa kwenye madawati,”alisema Mligo.
Viongozi wa chama cha waalimu CWT mkoa wa Njombe wanaona umuhimu wa kutoa elimu kwa waalimu wanawake na walemavu huku wakiwaelimisha juu ya sera ya elimu bure na mwenyekiti CWT Kitengo ke taifa anaomba uwiano urekebishwe.
Katibu wa chama cha waalimu mkoa wa Njombe Fratern Kwahison anasema kuwa waalimu baada ya kupatiwa maada mbalimbali kuhusiana na elimu bure wameibua changamoto mbalimbali na kuomba serikali kukaa na wadau hao ili kuangalia namna ya kuzitatua.
Aidha mwenyekiti wa CWT kitengo cha wanawake Sherida Mtaki, anaomba serikali kuhakikisha kuwa inatafuta ufumbuzi wa tatizo la uchache wa waalimu baada ya kuanza elimu ya bure wanafunzi wengi wamejiandishisha na kuwazidia waalimu.
“Sasa serikali ifanye jitihada za kuongeza waalimu na madarasa ili kuweka sawa uwiano wa waalimu na wanafuzi nashukuru wazazi wamepokea vizuri suala la kuwapo kwa elimu bure wamepeleka watoto wao shule,”alisema Mtaki.
Victoria Kiwale, ni mwalimu wa wanafunzi viziwi 
Katibu wa chama cha waalimu mkoa wa Njombe Fratern Kwahison

from Blogger http://ift.tt/2amagNX
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/29NNwL4

No comments:

Post a Comment