Tuesday 10 May 2016

Mwalongo Mshinde kesi ya kupinga matokeo jimbo la Njombe kusini


MAHAKAMA kuu kanda ya
Iringa imemtangaza Edward Mwalongo Kuwa mbunge wa jimbo la Njombe kusini katika
kesi iliyo kuwa ikimkabili ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyo funguliwa na
aliye kuwa mgombea ubunge kupitia Chadema Emmanuel Masonga.
Akisoma hukumu hiyo ya
kesi namba 5 ya uchakuzi mwaka 2015 jaji wa mahakama hiyo Jaji Jacob Mwambegele
alisema kuwa baada ya kupitia ushahidi ulio tolewa mahakamani hapo unaonyesha
kuwa mlalamikaji hakupeleka malalamiko yake katika kamati ya ya maadili ya
uchaguzi ya jimbo.
Alisema kuwa mahakama
yake haiwezi kutengua ushindi uliomtangaza mbunge wa jimbo la Njombe Kusini kwa
kuwa mdai hakupeleka malalamiko yake katika kamati ya maadili kama sheria
inavyo sema.
Jaji Mwambegele
alisema kuwa licha ya mahakama yake kubaini kuwapo kwa kampeni zilizo kuwa
zemekiuka misingi ya kimaadili na kuendeshwa kwa udhalilishaji lakini
mlalamikaji hakufuata sheria ya uchaguzi.
Alisema kuwa kigezo
cha kuto peleka malalamiko katika kamati ya maadili Masonga inamnyima haki ya
kupinga matokeo hayo kwa kuwa kamati ya maadili ilikuwepo na kuunyima ushahidi
wake nguvu ya kushinda.
Jaji Mwambegele
alisema kuwa uchaguzi huo uliendeshwa kwa uhuru na haki na kuwa hawezi kumtegua
mshinde aliye shinda katika uchaguzi huo.
Kesi hiyo ilisikilizwa
mashahidhi zaidi ya 30 kutoka pande zote za walalamikaji na washitakiwa na
kusikilizwa kwa zaidi ya miezi 3 huku baadhi ya wiki kuendeshwa mfurulizo bila
kupumzika na kufanya kesi hiyo kuisha haraka.
Katika ukumbi wa
mahakama wafuasi wa Chadema walionekana kuwa wengi kuliko wale wa Chama cha
mapinduzi CCM ambao walifika kusikiliza hukumu hiyo.
Aidha mbunge Mwalongo
alitoa shukrani zake kwa mahakama Kuu kwa kumtangaza mshinda katika kesi hiyo
ya kupinga matokeo.
Octoba 25 mwaka huu
kulifanyika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani ulimtangaza Edward
Mwalongo kuwa mshindi wa kiti cha ubunge katika jimbo la Njombe Kusini ambako
kulikuwa na wagombea wane ambao walisimamishw ana Vyamba vya CCM, Edward
Mwalongo kura 27285, Chadema Emmanuel Masonga kura 23003, Act Wazalendo Emilian
Msingwa kura 3888 na DP William Myegeta. kura 94 katika kata zake 13

from Blogger http://ift.tt/1Xj2dVm
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/27awqKJ

No comments:

Post a Comment