Tuesday 10 May 2016

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe awataka bodaboda kwenda shule ndani ya miezi 2



KAMANDA  wa  polisi
mkoa wa Njombe Pudensiana Protas ametoa miezi miwili kwa madereva Bodaboda mkoa
wa Njombe kupata mafunzo ya udereva kabla hawajaanza kuwakamata wale watakao
wabaini hawajapata mafunzo wala kuwa na reseni ikiwa ni mkakati wa kupambana na
ajali zinazoweza kuzuilika zinazo sababishwa na pikipiki.

Kauli hiyo
ameitoa wakati akifunga mafunzo kwa madereva Bajaji na pikipiki maarufu
Bodaboda 320 halmashauri ya mji Makambako ambao wamepatiwa mafunzo hayo na
Taasisi ya Apec kwa muda wa wiki moja baada ya wiki iliyo pita kumaliza mafunzo
hayo madereva 300 na kufikia jumla ya madereva 620.
Protas
alisema kuwa anatoa miezi miwili madereva hao kupata mafunzo ili kuanza
kuwasaka ambao hawana reseni za kuendesha pikipiki za mataili matatu (Bajaji)
na magurudumu mawili (Bodaboda) ambao wamekuwa wakijifunza mitaani na kuingia
barabarani na kusababisha ajali.
Madereva hao
wametoka katika maeneo matatu tofauti ya halmashauri ya Makambako mjini na
maeneo ya Pembezoni kwa halmashauri hiyo.
Alisema kuwa
sasa amepata waalimu zaidi ya 600 ambao watakuwa ni mabarozi na kuwaelimisha
wengine kuhusiana na usalama Barabarani na anaamini walio pata mafunzo watakuwa
chachu ya kupunguza ajali za barabarani.
Aidha
mkurugenzi wa taasisi hiyo ya Apec, Respisius Protas ameiomba serikali
kuhakikisha kuwa inawajengea vijana wa bodaboda vibanda maeneo ya kuegesha
Pikipikizao ili kujiongezea kipato kama halmashauri kwa kuwa wakiwajengea
maeneo ya kuegesha wataenda kuchukua ushuru hapo.
Alisema kuwa
madereva hao wamekuwa wakikosa maeneo ya kuegesha vyombo vyao na wakiwa na eneo
la kuegesha lina kuwa halina kibanda ambapo kipindi cha mvua hunyesewa na
likiwaka jua ni lao.
Alisema kuwa
kupitia mafunzo hayo madereva hao wamepata mafunzo ya ujasiliamali na
uendeshaji salama wa pikipiki na kuiomba halmashauri kutenga asilimia 5 ya
mapato yake kwaajili ya madereva hao kukopeshwa kwa riba nafuu.

from Blogger http://ift.tt/1T8I6GF
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/1TCfToA

No comments:

Post a Comment