Tuesday 26 April 2016

Madiwani walalamikia kuwapo kwa Rushwa ya maandazi kutoka kwa mamalishe Makambako

MADIWANI wa halmashauri
ya mji makambako mkoani Njombe wametakiwa kutoa elimu kwa wananchi ili kuacha
tabia ya kuuza ardhi na kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima kutokea katika
ameneo yao.
Hayo
yamebainisha na Bathoromeo Mwelange afisa tarafa ya Makambako kwa niaba ya mkuu
wa wilaya Njombe katika kikao cha robo ya mwaka cha baraza la madiwani wa
halmashauri hiyo.
Mwelange alisema
ushirikishwaji ukiwepo kati ya viongozi na wananchi migogoro inaweza kutatuliwa
mapema pasipo kuleta madhara
Alisema kuwa
wananchi wamekuwa wakiuza Ardhi kwa kazi kwa wageni kitu ambacho kisipo tiliwa
maanani kunaweza kukatokea shida ya ardhi kwa wazawa wa maeneo ya kata zao.
“Ardhi
inauzwa bila mpangilio huko vijijini kitu kinacho weza kuleta mtafaruku hapo
baadae kwa kuwa watoto wao wanao wazaa sasa walioko shule watashindwa mahara pa
kujenga na maeneo ya kulima chakula hayata kuwepo na kutakuwa na wageni wengi
kuliko wenyeji, madiwani toeni elimu kwa wananchi wenu wapunguze kasi ya kuuza
Ardhi,” alisema Mwelange.
Awali
akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Chesco Mfikwa aliwataka
madiwani wa halmashauri hiyo kukemea vitendo viovu ikiwemo tabia ya kutoa na
kupokea rushwa.
Alisema kuwa
Rushwa imetawaliwa katika kila sehemu ya mji huo ambapo kumekuwa na wananchi
wanao pokea rushwa na kutoa wote wanatena kosa.
“Kumekuwa na
shida kwa migamo wa mji ambao wanapokea rushwa kwa mama Lishe na kuendesha
maisha yao ya kupokea rushwa madiwani hakikisheni vitendo hivyo haviendelei,
mamalishe hakikisheni mnadai lisiti kwa kila azabu mnayo pewa na afisa yoyote
wa serikali,” alisema Mfikwa.
Hata hivyo
baadhi ya madiwani walisema kuwa wamekuwa wakishihudia wananchi wakitoa rushwa
ya chai na maandazi kwa Migambo hasa wanapo enda kuwakamata kutokana na Uchafu.
Diwani Baraka
Kivambe diwani wa kata wa magegere alisema kuwa migambo wamekuwa wakipokea
rushwa ya chai na maandazi asubuhi wanapo mamalishe, huku akusema kuwa wagaguzi
wa nyama wamekuwa wakihongwa kilo za nyama wanapo enda kukagua nyama katika
machinjia ya Makambako.
Aidha Diwani
wa kata ya Mizani Perepetua Ngongi alisema kuwa kumekuwa na shida ya migambo
kupokea rushw akwa madereva bajaji na kuweka bajaji zao mahara palipo katazwa
na kuwa halmashauri iliweka azimio la kuwatoza faini madereva hao lakini
kuwekuwa na uendelezwaji wa vitendo hivyo.
Aidha
madiwani hao waliiomba serikali ya mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa
makambako kuwawajibisha watendaji wabadhirifu kufuatia kudhoofisha mwenendo wa
ukusanyaji mapato ya serikali ya halmashauri yao.

from Blogger http://ift.tt/1reBJbp
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/1qOZciO

No comments:

Post a Comment