Tuesday 26 April 2016

Madaktari bingwa watano watua njombe watatibu wagonjwa kwa siku tano

WIZARA ya
afya, maendeleo ya jamii ,jinsia watoto na wazee, kupitia mfuko wa bima ya afya
ya taifa NHIF imekabidhi madaktari bingwa watano wa magonjwa ya Moyo, Usingizi
watoto na uzazi kwa wakina mama, katika hosptali ya mkoa wa Njombe kibena ambao
watahudumu kwa siku tano.
Madaktari
hao wameanza kutoa huduma ya afya kwa kushirikiana na wataalamu wa
hospitali ya kibena mkoani Njombe kwa muda wa siku tano kwa kutibu magonjwa ya
ndani ya moyo, usingizi (nusu kaputi) watoto na uzazi kwa akina mama.
Akiwakabidhi
madaktari hao mkoani Njombe Mkurugenzi wa matibabu na huduma za kiufundi makao
makuu NHIF Dr Frank Lekey alisema huduma hiyo kwa mkoa wa Njombe ni ya 16 na alikabidhi
dawa na vitendanishi kwaajili ya kupimia magonjwa mbalimbali.
“Huduma hii
tunaitoa mkoa wa Njombe ikiwa ni ya kumi na sita kutolewa hapa nchini na pia
katika hospitali hii ya Kibena tunakabidhi dawa pamoja na Vitendanishi wa
kupimia magonjwa mbalimbali hospitalini hapa” alisema Dr. Lekey.
Akizundua
mpango huo kwa niaba ya katibu mkuu wa wizara ya afya Dr. Mpoki Ulisubisya, mganga
mkuu wa Hospitali nchini Prof. Mohamed Bakari alieleza dhamira ya wizara na
mfuko kuwa ni kuifikia jamii kubwa kwa urahisi kwa kuwasogezea Madaktari katika
ngazi ya mkoa.
Prof. Bakari
pia alitoa wito kwa wananchi kujiunga kwa wingi na mfuko huo wa afya ili
kuendelea kupata huduma za afya bure pindi wanapo ugua kuriko wakisubili
kulipia wakiwa wanaumwa.
“Wananchi
jiungeni na mifuko ya bima ya afya kwa kuwa katika mifuko hii mnawekeza pesa
kwaajili ya kutibiwa ukiugua kwa kuwa ugonjwa hauchagui sasa una pesa ama hauna
kwa hiyo unaweza kuugua wakati hauna pesa na ukashindwa kununua dawa” aliongeza
Prof. Bakari.
Aidha NHIF
Imekabidhi dawa na vitendanishi kwa hospitali hiyo vyenye thamani ya shilingi
milioni tano ambapo mganga mkuu wa mkoa wa Njombe Dr Samweli Mgema akitumia
fursa hiyo kuushukuru mfuko wa bima ya afya NHIF kwa kuwapatia dawa hizo.
Kwa upande
wao wananchi wa Mkoa wa Njombe wameishukuru serikali kupitia NHIF kwa  Kusogeza huduma hiyo ya madaktari bingwa
ambayo kabla wamekuwa wakiipata nje ya mkoa tena kwa gharama kubwa na kuwa
wamekuwa wakilazimika kwenda jijini Dar Kwaajili ya kutibia magonjwa ya moyo.

from Blogger http://ift.tt/1NOo7Z9
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/1qOZciW

No comments:

Post a Comment