Wednesday 16 March 2016

Diwani azuia uhamisho wa mtendaji alodaiwa mbadhilifu

DIWANI  wa kata ya Lupombe  amezuia uhamisho wa mtendaji wa kijiji cha Luponde  Wilayani Njombe  Stiniususi Mlowe anaye daiwa kukuhusuka na upotevu wa fedha za vocha za Ruzuku za pembejeo za zaidi ya milioni tatu  mpaka atakapo zilejeha.
Fedha hizo zinadaiwa kuwa ni za vocha 40 za ruzuku ya pembejeo za kilimo katika vijiji vya Luponde na Lusitu ambapo vicha hizo zilitakiwa kupatiwa wananchina kaya masikini.
Akizungumza na wananchi  diwani wa kata ya Luponde  Ulrick Msemwa  alisema  kufuatia matumizi mabaya ya  vocha za pembejeo  za kilimo  yaliofanywa na mtendaji huyo, afisa utumishi wa halmashauri ya mji wa Njombe  hatakiwi kumuhamisha   hadi  atakapo maliza malipo  ya fedha shilingi milioni mbili na laki nne za kijiji cha Luponde na shilingi laki 8 za kijiji cha Lusitu sawa na shilingi milioni tatu na laki mbili.
Katika kikao hicho wazazi wa mtendaji huyo baada ya kukili kuwapo kwa ubadhirifu huo wazazi wake wameamua kulipa fedha hizo ndani ya siku 30.
“Vocha hizo zitalipwa ndani ya siku 30 na fedha hizo zitalipwa na wazazi wa afisa mtendaji, na baada ya hapo fedha zizo zitafanya kazi zingine baada ya kurejeshwa na wazazi tuwe tunawauliza watoto wetu amefanya kazi mda mfupi anamali zinazo zidi mshahara tuwaulezi wasio endelea tusiwashangae,” alisema Msemwa
  
Hata hivyo licha ya vocha hizo kutakiwa kutumika kwaajili ya wananchi na kaya zilizo na uwezo duni kwaajili ya kulipa pembejeo za kilimo lakini wanadaiwa kupewa watu wenye uwezo na watumishi wa umma.
Mtendaji huyo alisema kuwa vocha hizo alizigawa kwa mratibu elimu kata, afisa mifungo, mwalimu mkuu wa sule ya Luponde, afisa afya, na kuna baadhi ya watu wa chama cha mapinduzi kupatiwa, na kuwa yeye mwenyewe alijigawia.
Wakizungumza kwenye kikao kifupi katika ofisi ya serikali ya kijiji cha Luponde baadhi ya wananchi na wajumbe wa serikali ya kijiji hicho wamesema kutokana na  wazazi  wa afisa mtendaji wa kijiji hicho kukili kulipa fedha hizo  ndani ya siku 30 baada ya kujiridhisha kuwa mtendaji huyo anamakosa  wanaomba Halmashauri kutohamishia  sehemu nyingine  kuendeleze tabia hizo  wanaobainika na tuhuma za ubadhirifu.
Hata hivyo halmashauri tayari imetoa uhamisho kwa mtendaji huyo licha ya kutuhumiwa kuhusika na wizi huo amekili kupewa barua  ya uhamisho  na afisa utumishi  wa halmashauri ya mji wa Njombe kuhamia kijiji cha Uliwa  na  wa Uliwa kuhamia kijiji cha Luponde  uhamisho wa kawaida si  kwa vile ametuhumiwa.

from Blogger http://ift.tt/22lDsck
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/1pL6WlQ

No comments:

Post a Comment