Kasmishna mkuu wa Idara ya Umoja wa Mataifa (UNHCR)
inayowashughulikia wakimbizi Antonio Guterres ameuomba umoja wa ulaya
kuwapokea wakimbizi 200,000.
Amesema kupokelewa huko kuwe chini ya mradi mkubwa wa kuwapatia
makazi ili kupunguza wimbi la wahamiaji wanaofika kwenye mipaka ya
nchi za Umoja wa Ulaya ili kutafuta hifadhi.
Mkuu huyo wa UNHCR ametoa taarifa mapema Ijumaa akiomba Umoja wa
Ulaya kutekeleza mradi ambao utahitaji ushirikiano wa mataifa yote ya
Umoja wa Ulaya.
Guterres amesema mataifa ya Ulaya yatapaswa kusaidia wakimbizi kwa kuwapatia hifadhi zinazostahiki.
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, amebadili
msimamo wake Ijumaa na amesema kuwa nchi yake itawakaribisha maelfu ya
wakimbizi zaidi.
Bwana Cameron, amesema wakimbizi ni wale kutoka Syria, na zaidi ya wale 5000 waliokwisha pokelewa hadi sasa.
Pia amesema hio ni kutokana na kuongezeka kwa janga na mateso wanopitia wakimbizi.
Kauli hiyo ilikuwa ni baada ya kufanya mkutano na Waziri Mkuu wa Ureno huko Lisbon, Ureno.
from Blogger http://ift.tt/1EIzMd1
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/1IRAsb3
No comments:
Post a Comment