kikosi cha AMISOM waliuwawa baada ya kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab
kushambulia kituo cha jeshi la Umoja wa Afrika katika mji wa Janale,
kusini mwa Somalia siku ya Jumanne.
Msemaji wa jeshi la Uganda, Paddy Ankunda alisema katika mtandao
kwamba miili 10 ilisafirishwa kutoka Mogadishu kwenda Uganda Alhamisi.
Bwana Ankunda alisema AMISOM iliwatambua wanajeshi wote na hakuna
mwanajeshi aliyepotea kutoka kituo cha Janale, kilichopo kilomita 120
kusini-magharibi mwa Mogadishu.
Wanamgambo wa Al-Shabaab walidai kiasi cha wanajeshi wa Uganda 70
waliuwawa katika shambulizi la Jumanne lakini vyanzo vya Sauti ya
Amerika-VOA vilisema jumla ya idadi ya vifo vya wanajeshi ni 20.
Msemaji huyo wa jeshi la Uganda alisema “shambulizi hilo limebadili
mtazamo” na al-Shabaab watarajie “majibu muafaka” kutoka kwa wanajeshi
wa Uganda. Bwana Ankunda aliongeza kwamba licha ya shambulizi, “Uganda
haitasitisha juhudi zake za kusaidia kuleta amani nchini Somalia”.
Wakati huo huo mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini Uganda, Jenerali
Edward Wamala alitembelea wanajeshi wa mstari wa mbele katika mji wa
Janale mahala ambapo alikutana na UDPF na kuwapongeza kwa azma yao ya
mapambano wanayofanya dhidi ya wanamgambo wa Al-Shabaab ambao
walishambulia kituo hicho.
from Blogger http://ift.tt/1EIzKBS
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/1IRAuj5
No comments:
Post a Comment