Friday 14 August 2015

Wanafunzi njombe waishauri seikari kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa

MWANAFUNZI wa shule za
sekondari za Njombe Sekondari na Uwemba wameiomba serikali kusimamia sheria ya
panda miti na kata miti kwa lengo la kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa
yanayo leta madhala mbalimbali duniani.
Wakizungumza baada ya
kupatiwa elimu juu ya madhala ya mabadiliko ya hali ya hewa iliyo tolewa na
mamlaka ya hali ya hewa Tanzania kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, waliwema kuwa
ili kukabiliana na hali ya hewa ni lazima sheria ziwe na meno ili kupambana na
mabadiliko hayo.
Mwanafunzi wa shule ya
Uwemba Mkoani Njombe Salafina Jailo alisema kuwa serikali inatakiwa kuhakikisha
kuwa kunautaratibu wa kuwabana wanao haribu mazingira bila  ya
kurudishia uharibifu wake.
Alisema kuwa kuna sera
ya panda miti kata mti haitekelezi kwa kuona watu wakikata miti na kuto panda
mti kitu kinacho sababisha ardhi kupoteza uoto wa asili na kusababisha ongezeko
la joto duniani.
“Kutokana na kuto
kuwapo kwa utekelezeji wa sera ya udhibiti wa uharibifu wa mazingira serikali
inaanza kupoteza vivutio vya utalii kama kuyeyuka kwa Barafu katika mlima
kilimanjaro na kusababisha watalii kupungua na kuikosesha serikali mapato,”
alisema Jailo.
Naye Festo Amanyisye
mwanafunzi wa Uwemba, alisema kuwa ongezeko la joto na upungufu wa mvua hasa
unasababisha na uharibifu wa mazingira unao tokana na ongezeko la viwanda na
kuwa serikali inatakiwa kuchukua juhudi za makusudi kuielimisha jamii kuhusiana
na utunzaji wa mazingira.
“Serikali inatakiwa kutekeleza
sera ya Panda miti kata mti ili kurejesha hali ya hewa ya zamani na kuwa watu
wanao kiuka sera hiyo kupewa adhabu ambayo itakuwa Mfano kwa wananchi wengine,”
alisema Amanyisye.
Aidha Ngalaba Sospeter
mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Njombe (Njoss) ameitaka serikali kuongeza
juhudi za kutoa elemu kwa umma hasa katika shule mbalimbali ili kuifikishia
elimu kwa jamii kwa urahisi hasa madhara ya uharibifu ili kuibadilisha jamii.
Hata hivyo Frederick
David mwanafunzi wa Njoss alisema kuwa kupitia elimu aliyo ipata kutoka kwa
mamlaka ya hali ya hewa atakuwa barozi wa kuhakikisha anapambana na mabadiliko
ya hali ya hewa ka kuhakikisha vitu vinavyo zuilika anashawishi kuvizuia.
Akizungumza baada ya
kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule hizo za Mkoani Njombe Mkurugenzi wa utafiti
na matumizi ya hali ya hewa Tanzania Dr. Ladslaus Chang’a , alisema kuwa
serikali kupitia mamlaka ya hali ya hewa imeanza kutoa elimu kuhusiana ana
mabadiliko ya hali ya hewa ili kupambana na madhara yanayo jitokeza kila mwaka.
Alisema kuwa
mabadiliko ya hali ya kewa yamekuwa yakisababisha kutokea kwa madhala
mbalimbali kama mafuliko na kusababisha vifo, ukame na kusababisha vivyo vya
wanyama huku elimu ikilenga upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira.
 Alisema kuwa
mamlaka hiyo imenzisha mfumo wa kutoa elimu na utabili wa hali ya hewa kwa njia
za ujumbe mfupi kwa wananchi na wakulima wanao tegemeo kulima kwa kutumia
utabili wa hali ya hewa hapa nchini.
Chang’a alisema kuwa
elimu hiyo inatolewa kwa wanafunzi mashuleni kwa lengo la kuwajenga wakiwa bado
mashuleni ili kuelemisha wazazi wao na kuwa na kizazi chenye elimu ya utunzaji
wa mazingira.




from Blogger http://ift.tt/1HM4iNu

via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/1WpS9sR

No comments:

Post a Comment