Monday 24 August 2015

Ushindi wa Magufuli utaletwa na Ukawa


Kwa muda mrefu nimekua nikifuatilia pilika pilika za vyama vya siasa kuelekea October ambapo utafanyika uchaguzi mkuu, na kupata rais wa awamu ya tano. Kwa mtazamo wangu ukawa watashindwa vibaya na Mh. John Pombe Magufuli. Sababu kubwa ninazoziona ni hizi hapa.

1. Ukawa ikiongozwa na chama kikuu cha upinzani kimekosa sura ya kitaifa
Kwa kiasi kikubwa viongozi wa ukawa hususani chadema kilichotoa mgombea urais kimekosa sura ya kitaifa. Viongozi wengi wa chadema wanatoka kaskazini, hii ni weakness kubwa sana kisiasa,, chama cha siasa kwa mazingira ya Tanzania kama kinataka kuchukua dola ni sharti kiwe chama cha siasa chenye sura ya kitaifa ili kipate support kutoka sehemu mbalimbali ya jamhuri ya muungano.

2. Dhana mfu ya mabadiliko
Kwa mtu mwenye civic competence kubwa na anauwezo mkubwa wa kuchambua mambo atakubaliana na mimi hakuna uhusiano wowote wa maana kati ya kubadili chama ili upate mabadiliko, nakubali kabisa kua na upinzani wenye nguvu ni kitu bora katika kujenga utawala bora lakini uhusiano na mabadiliko ni mdogo au hakuna kabisa. Nitatoa mfano: Japani toka mwaka 1955 kimeongozwa na chama kimoja cha siasa LDP TOKA mwaka 1955 mpaka 1993 kikatolewa madarakani kwa mda wa miezi 11 kikarudi tena madarakani mwaka 1994 mpaka 2009 kikatoka tena madarakani, mwaka 2012 kikarudi tena mpaka leo. LPD ndio chama kilicholeta mabadiliko makubwa ya kiuchumi kutokana na sera nzuri za kujenga uchumi. Chama cha kikomunisti cha China kimekaa mda mrefu sana na CHINA ipo hapo ilipo leo.

Tatizo kubwa la UKAWA ni kudai mabadiliko kwa kuwaaminisha wananchi kwamba CCM ikitoka madarakani maisha yatakua mazuri. Kuna tofauti kubwa ya ahadi, kwa maana ya kuleta mabadiliko na kuja na mikakati mizuri ya kiuchumi na kijamiii ili waaminiwe kuongoza nchi, sera zao hazieleweki na wanatumia matatizo ya vijana kwa kuwadanganya kua maisha yatabadilika CCM ikitoka madarakani.

3. Udhaifu wa Mgombea wa UKAWA
Ukawa nawamgombea urais dhaifu, hana uwezo wa kujenga hoja na haelezi vitu vya msingi ili kujenga uchumi na taifa hili na kuleta hayo “MABADILIKO” Lowassa kwa mda mrefu jukwaani ameshindwa kujieleza vizuri na nimtu anaeonekana ana matatizo ya kiafya, amekua haelezi nini atafanya zaidi ya kuhamasisha vijana wadai mabadiliko, LOWASSA NI DHAIFU SANA KUJENGA HOJA UKILINGANISHA NA JOHN MAGUFULI, hili litawaletea matatizo makubwa mbele ya safari kampeni zikipamba moto c z magufuli anauwezo mkubwa wa kujenga hoja na kuitetea vizuri.

Naomba kuwasilisha.

By Manelezu


from Blogger http://ift.tt/1Jgiany
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/1Jgkmex

No comments:

Post a Comment