URAFIKI WAANZIA KWENYE KAMPENI ZA CCM
Mastaa hao walianza kuwa na ukaribu mkubwa kwenye mambo ya Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizozinduliwa Jumapili iliyopita katika Viwanja vya Jangwani, Dar.
Habari zilieleza kwamba, kabla ya hapo, wawili hao hawakuwahi kuwa na urafiki hata zaidi ya salamu.
WEMA AMPOZA BATULI
Chanzo ambacho ni mtu wa karibu na wawili hao kilieleza kwamba, baada ya Batuli kupata mkasa wa kuunguliwa nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya …Mbezi Beach, Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita, mastaa hao walikuwa wote saluni na walipopata taarifa ya mkasa huo, Wema ndiye aliyempooza machungu Batuli kwa kumsaidia katika kipindi kigumu alichokuwa nacho.
“Wema aliamua kumsaidia Batuli na inasemekana kwa sasa anaishi naye nyumbani kwake, Kijitonyama (Dar),” kilidai chanzo hicho.
HOFU YA UFAFIKI WAO
Ilidaiwa kwamba, hofu ya urafiki kwa mastaa hao imetanda kwa baadhi ya mashabiki wao kwa kuwa, kila mmoja anapenda kuwa juu ya mwingine hivyo urafiki huo unazua wasiwasi kama wanaweza kudumu kwa muda mrefu kutokana na tabia zao kushabiana na kuleta maana halisi ya methali kuwa mafahari wawili hawawezi kuishi zizi moja.
“Kwa kweli Batuli na Wema kuwa marafiki ni ngumu kwa kuwa kila mmoja hapendi kujishusha kwa mwenzake, kitu ambacho kitafanya urafiki wao kuvunjika muda si mrefu,” kilidadavua chanzo hicho kwa sharti la kutochorwa gazetini.
YASIJE KUWA YA SNURA, KAJALA, AUNT
Kuhusiana na urafiki huo, minong’ono imekuwa mingi kwamba, kwa nyakati tofauti, Wema amekuwa na marafiki wengi lakini wote aligombana nao kwa madai kuwa huwa hawezi kudumu na rafiki wa kike kwa muda mrefu kama anavyoweza kudumu na marafiki wa kiume kama ilivyo kwa Petit Man, Martin Kadinda na Mirror.
Wawili hao walipotafutwa ili kutia neno katika urafiki wao hawakupatikana.
from Blogger http://ift.tt/1JkNajU
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/1Kmi3ZK
No comments:
Post a Comment