Monday, 10 August 2015

Bvr njombe tena, uhakiki wa taarifa

HALMASHAURI ya wilaya ya Njombe imepokea mashine mbili za
kuandikishia mpigakura kwa mfumo wa kierekroniki, (BVR) kwaajili ya kufanya
marekebisho ya watu ambao walijiandikisha kupigakura na taarifa zao kukosewa.
  
Akizungumza ofisini kwake kaimu Mkurugenzi halmashauri ya
mji wa Njombe na afisa utumishi Mbujilo Gwarbet, alisema kuwa halmashauri hiyo
imepokea Bvr mbili kwaajili ya kufanya uhakika na kurekebisha wale ambao majina
yao yatakuwa yamekokewa na kuwa ambao wamehama maeneo kurekebishiwa kulingana
na na eneo alilopo.
Alisema kuwa kwa mashine hizo kila kata itapata mashine moja
ambayo itakaa katika kata husika kwa muda wa siku tano ambapo mkazi wa eneo la
kata hiyo ataenda katika ofisi ya kata ambapo mashine itakuwepo kwenda kufanya
marekebisho.
“Mashine hizi zimekuja kwaajili ya kufanya marekebisho kwa
watu ambao wanaona wamehama maeneo yao na kuona majina yalikosewa, au jina la
kituo chake lilikosea watabadilisha lakini kwa wale ambao hawakujiandikisha
hawata andikishwa labda kama kitambulisho kilipotea lakini alijiandikisha”
alisema Gwalbet.
Alisema kuwa kwa wale ambao vitambulisho vilipotea watapewa
vitambulisho vipya kwa kuvifuta katika orodha vile vya zamani na kuwa kama mtu
alihama mkoa, kata ama mtaa atabadilishiwa taarifa na kuwekewa taarifa za kata
aliyopo na kuwa itaangaliwa kama mwaka wa kuzaliwa ulikosewa..
Alisema mashine hizo kwa halmashauri yake zimeza kufanya
kazi Ijumaa Augosti 7 ya mwishoni mwa wiki na itaendelea mpaka Septemba 10 na
kuwa umeanza katika kata za Kifanya na Kihungilo ambapo mashine zitadumu kwa
siku tano.
Baada ya kutoka katika kaza hizo na kumaliza siku tano
mashene zitahamia katika kata za Makoho na Matola,zoezi litaanza Agosti 12 hadi
16, na kwa awamu ya tatuitakuwa ni kata za Lupondena Uwemba itakuwa ni Agosti
17 hadi 21 na Lugenge na Utalingolo Agosti 22 – 26,kata  Ihanga na Yakobi itakuwa Agosti 27- 31.
Aliongeza kuwa katika kata za Mjimwema na Ramadhani itakuwa
ni Septemba 1 – 5 na kuwa zoezi hilo litamalizikia katika kata ya Njombe mjini
Septemba 6 hadi 10 ambapo jimbo hilo la Njombe kusini litakuwa limemaliza uhakika
wake kwa kata zote 13.
 Gwalbert alisema kuwa
pia katika uhakika huo utakuwa unatoa watu ambao wamefariki katika Daftari na
kuwato wale ambao wamepata matatizo ya kufungwa kuondolewa katika Daftari hilo.

from Blogger http://ift.tt/1IxxICU
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/1TjxP7W

No comments:

Post a Comment