Friday 17 March 2017

WATU WATANO HATARI WALIOWAHI KUISHI

Hapo zamani wawindaji, maharamia na wanajeshi waliheshimiwa sana katika jamii. Walisifiwa sana na walikuwa wakionekana kama mashujaa.
Baadhi ya mashujaa waliongoza majeshi, wengine waliwawinda wanyama hatari na wengine walitawala makasri kama maharamia.
1
Kama ungependa kujua Zaidi kuhusu baadhi ya wawindaji mashuhuri, wapelelezi na wanajeshi wa zamani, hii hapa ni orodha ya mashujaa watano waliowahi kuwepo.
1. Madame ching au Ching Shih, alikuwa ni mmoja wa maharamia aliyewahi kuiongoza bahari ya China katika karne ya 19. Madame Ching alianza kama mwanamke anayejiuza, lakini baadae aliolewa na haramia. Madame Ching pia ni mmoja kati ya maharamia wachache sana waliowahi kustaafu kutoka uharamia.
Haramia aliyemuoa Madame Ching alikufa katika tsunami na nafasi yake ilichukuliwa na mkewe. Aliivuruga bahari ya uchina na kushinda vita nyingi alizopigana. Alipigana dhidi ya himaya nyingi kupita kiasi ikwemo Ureno, Uingereza na nasaba ya Qing.
Aliyashinda majeshi mengi na himaya nyingi. Amewahi pia kumteka afisa maarufu Richard Glass Poole pamoja na mabaharia wengine saba mnamo mwaka 1809. Alipata msamaha mwaka 1810 na kufariki mnamo mwaka 1844 akiwa na umri wa miaka 69.
Alichukuliwa kuwa mmoja kati ya maharamia wanawake waliokuwa maarufu na wenye nguvu sana katika historia.
2. Leo Major, alikuwa mwanajeshi kutoka Ufaransa na Canada aliyepigana vita ya pili ya dunia. Ni raia wa Canada pekee katika historia aliyepokea tuzo mbili za “Distinguished Conduct” katika vita mbili tofauti.
Mwanajeshi huyu aliyejulikana sana na alipoteza jicho lake moja katika vita alipotupiwa bomu la mkono na alikuwa akifananishwa na haramia.
Mnamo mwaka 1945, Meja aliteka mji wa Zwolle kutoka kwa wanajeshi wa kijerumani na alipokea tuzo yake ya kwanza. Wakati wakifanya mipango ya upelelezi na Koplo Willie Arsenault, wanajeshi hawa wawili walipanga kuuteka mji. Willie aliuawa, lakini Meja aliendelea na mpango wake. Aliingia mjini kwa fujo huku akiipiga bastola yake kwa vurugu pamoja na kutupa mabomu ya mkono.
Wanajeshi wa kijerumani walidhani kuwa jeshi la Canada linaushambulia mji, wakakimbia. Siku hiyo Meja aliwakamata wanajeshi zaidi ya 1800 na kuwauwa wengi Zaidi. Aliipokea medali yake ya kwanza ya “Distinguished conduct” kwa ushindi wake wa kushangaza.
Meja aliipata medali yake ya pili ya “Distinguished conduct” wakati wa vita ya Korea kwa kupigana vita ya kwanza ya Maryang San, ambapo aliuteka na kuushikilia mlima muhimu.
3. Jack Churchill, ambae alijulikana pia kama “Mad Jack”. Churchill ambae alikuwa afisa wa jeshi la Uingereza, maarufu sana kwa kupigana vita ya pili ya dunia akitumia sime ya Kiskochi, upinde mrefu pamoja na mishale.
Huyu ni maarufu kwa wito wake uliosema kuwa “Afisa yeyote anaeenda katika kazi pasipokuwa na upanga wake basi huyo hajavaa vizuri.” Mwaka 1943, Churchill aliongoza wanajeshi kutoka Sicily akiwa na upanga wake ulioning’inia kwenye mkanda , upinde na mishale pamoja na filimbi yake mkononi.
Aliupiga mji na kuwateka wafungwa 42 na kurudi kuchukua upanga wake alioupoteza wakati wa mapambano. Ilipoisha vita ya pili ya dunia mnamo mwaka 1945, Churchill hakuridhika hata kidogo, alinukuliwa akisema kuwa “kama siyo hawa Wamarekani, tungeiendeleza vita hii kwa miaka mwingine 10.”
4. Jim Corbett alikuwa mwindaji maarufu aliyekamata duma na chui wengi huko India katika miaka ya 1907 mpaka 1938.
Inasemekana kuwa amewahi kutega na kuwaua duma 19 na chui 14 waliokuwa wakiwadhuru watu katika kazi yake ya uwindaji. Corbett alikuwa pia ni Kanali wa Jeshi la Uingereza huko India. Amewahi kuitwa ili awaue chui waliokuwa wakiwawinda na kuwajeruhi watu.
Ameandika vitabu kadhaa kuhusu uzoefu wake wa kuwinda. Katika maisha yake ya baadae alikuja kuwa mpigapicha na mhifadhi. Pia alikuwa msemaji wa ulinzi wa wanyamapori nchini india.
5. Hugh Glass, huyu alikuwa mpelelezi na muwindaji maarufu wa Marekani.
Mwaka 1823, alishambuliwa na kujeruhiwa na dubu. Rafiki zake wakiwa na uhakika kuwa amekufa walimtelekeza porini.
Hugh Glass alinusurika na kutambaa zaidi ya maili 200 kuelekea eneo salama kwa muda wa wiki sita pasipokuwa na chakula wala silaha yoyote.
Inasemekana alinusurika kwa kula mizizi ya miti na mimea mbalimbali pamoja na matunda. Wakati wengine wanasema kuwa aliua na kula nyoka wenye sumu kali (rattlesnakes).

from Blogger http://ift.tt/2nsdnNR
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2mTJAfa
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2mxrgFt
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2mzHhvf
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2mOEXla

No comments:

Post a Comment