Thursday 16 March 2017

WANANCHI WAVUNJA VYOO VYA SHULE YA MSINGI HUKO NJOMBE

VYOO vya shule ya msingi Ramazani vya zamani vimevunjwa na wananchi baada ya kuona vyoo vipya walivyo vijenga kwa nguvu zao havitumiki na wanafunzi wa shule hiyo ikisubiliwa kufunguliwa na mwenge wa uhuru kitu lilicho sababisha mwenyekiti wa mtaa huo na Diwani kuhojiwa na polisi kwa zaidi ya masaa mawili.
Walio hojiwa na polisi kwa zaidi ya masaa mawili ni pamoja na mwenyekiti wa kamati ya shule Diwani wa kata ya Ramazani na mwenyekiti wa mtaa huo huku kukidaiwa kuwa aliye enda polisi ni mkuu wa shule kwa shinikizo la afisa elimu.
Wananchi wakizungumzia kubomolewa kwa vyoo hivyo wanasema kuwa wameamua kubomoa vile vya zamani kwa lengo la watoto wao kuanza kutumia vile vipya.
Wananchi wanasema kuwa wamechoka kuwatibu watoto wao magonjwa ya mara kwa mara kutokana na kuwa na vyoo hivyo.
Diwani na mwenyekiti wanazungumzia kilichowapeleka kuhojiwa na polisi mbele ya wananchi.
Polisi iliingia katika shule ya msingi Ramadhani kwa lengo la kushuhudia vyoo vilivyo bomolewa na wananchi ili wanafunzi kuanza kutumia vipya baada ya kuikabidhi kamati ya shule siku tatu zililizopita lakini havijaanza kutumiaka kukidaiwa kuwa mpaka mwenge wa uhuru upite kuzindua mwezi April Mwaka huu ndipo vianze kutumika.

from Blogger http://ift.tt/2mxvRr1
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2n3S8k6
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2nsz1RW
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2m6GW7d

No comments:

Post a Comment