Sunday 19 March 2017

TzTown Tv: USHIRIKIANO NI SIRI YA KUWA NAFASI YA KWANZA KITAIFA NJOMBE MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

USHIRIKIANO baina ya wazazi na waalimu kunaweza kumfaulisha mwanafunzi ama kumfelisha katika mitihani yake ya elimu yoyote hasa ya msingi na sekodari kitu kinacho fanyika mkoani Njombe kwa shule zilizofanyavizuri ni ushirikiano mzuri kati ya wanafunzi na waalimu wao. 
Hayo yanabainishwa mbele ya mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka wakuu wa shule za sekondari mkoani Njombe ambao wanakutana katika umoja wao wa wakuu wa shule Nchini Tahosa ambao wanajadili masuala ya kuweka sawa elimu kwa shule za mkoa wa Njombe. 
Mwenyekiti wa Umoja huo mkoa wa Njombe anaeleza mafanikio yao na kuzitaja changamoto zinazo wakabili katika kutekeleza majukumu yao. 
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka anasema kuwa ufauru huo uendelezwe na kuwa shule kufanya vibaya sio kosa la mkuu wa shule na suruhu sio kumfukuza mkuu wa shule. 
Wakuu wa shule nao wanasema kuwa kilicho sababisha kufanya vizuri ni kuwapo kwa ushirikiano mzuri kati ya waalimu, wanafunzi na wazazi huku kukiombwa mabweni ambayo yatasaidia kuinua ufauru kwa shule nyinginezo. 
TAZAMA WALIMU WAKIZUNGUMZA NA MKUU WA MKOA MOJA KWA MOJA…………………..

from Blogger http://ift.tt/2nRJ7bi
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2nF9K3Y

No comments:

Post a Comment