Friday, 24 March 2017

TRA inaidai Tanesco shilingi bilioni 4

Shirika la umeme Tanzania (Tanesco), linadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 4 na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) za kodi ya mitambo ya kuzalisha umeme iliyokwama katika Mamlaka ya Bandari Tanzania.
Akizungumza na wanahabari Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Deo Ngalawa, baada ya kutembelea mradi wa uzalishaji wa umeme wa gesi asilia wa Kinyerezi, Dar es Salaam, alisema kuwa mitambo hiyo iliingizwa nchini ili kuongeza uzalishaji wa umeme.
“Tanesco inadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 4 na TRA, deni hilo linatokana na kukwama kwa mizigo ya kuzalisha umeme, ikiwamo mitambo na jenereta kutoka nje ya nchi, jambo ambalo linachangia kurudisha nyuma uzalishaji wa umeme,” alisema Ngalawa.
Aidha alisema maeneo mengi ya mradi huo yanahitaji kuwekwa mitambo ambayo imezuiliwa kutoka kutokana na deni hilo, hivyo watazungumza na serikali kuona namna ya kutatua changamoto hiyo.
TAZAMA JAMAA HUYU ALIVYOKOSWA KOSWA NA KIFO KWA AJARI MTONI

from Blogger http://ift.tt/2nkyoIX
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2nvMszT

No comments:

Post a Comment