Taarifa ya siku ya tatu ya ziara maalum ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe Januray Makamba kutembelea mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania yenye lengo la kung’amua changamoto za kimazingira, athari za mabadiliko ya tabia nchi ili kuweka mikakati sahihi ya kukabiliana na changamoto hizo.
Katika siku ya tatu ya ziara hiyo Waziri Makamba amepokea ripoti ya mazingira ya mkoa wa Tanga toka kwa mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella ambapo pia alikutana na kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira iliyo katika ziara ya kikazi mkoani Tanga.
Akianisha changamoto za kimazingira mkoani Tanga, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella ameeleza kuwa kuna athari kubwa za mazingira kutokana na ukataji miti hovyo, uchimbaji holela wa madini katika vyanzo vya maji na sehemu za milima ya Amani hasa eneo ambalo kunapatikana vyanzo vingi vya maji lakini pia uwepo wa madini katika eneo hilo unahamasisha uchimbaji unaoharibu mazingira.
Vilevile taarifa imeanisha changamoto kubwa zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi zinazopelekea maeneo ya nchi kavu yanayopakana na bahari kulika na maji kutokana na kuinuka kwa kina cha bahari akitolea mifano eneo la Raskazoni ambapo Bahari inakula eneo la nchi kavu karibu kabisa na barabara pamoja kisiwa cha wafu/kifo (Toten Island) ambacho kipo hatarini kupotea kutokana na kuinuka kwa kwa kina cha maji.
Baada ya kupokea taarifa hiyo Waziri Makamba alipata wasaa wa kutembelea na kukagua maeneno yanayotajwa kuathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi ya Raskazoni pamoja na kiswa cha wafu/kifo (Toten Island) ambapo ameahidi kutuma wataalamu watakaoshirkiana na wataalamu waliopo mkoani Tanga ambao baada ya kufanya upembuzi yakininifu watapendekeza hatua bora zaidi za kuchukua kukabiliana na changamoto hiyo. Vilevile ameagiza kufanyika operesheni maalum ya kupambana na wavuvi haramu wananaotumia baruti katika uvuvi jambo lenye athari kubwa sana mazingira ikiwemo kuua na kuharibu matumbawe ambayo ni moja ya tegemeo kubwa kwa mazalia ya samaki na ambayo huchukua mpaka miaka 70 kurudi hali yake baada ya uharibifu.
Waziri Makamba ameanisha umuhimu wa kuchukua hatua za haraka katika kukiokoa kisiwa cha Toten ambapo amesema hatua za haraka ni kujenga ukuta kama serikali ilivyofanya kwa sehemu za Dar es Salaam na Pangani.
Ameainisha kwa undani kuwa kisiwa hicho kina faida na umuhimu mkubwa sana kwa bandari ya Tanga, kisiwa hicho ndicho kinaikinga bahari ya Tanga dhidi ya mawimbi makubwa ya bahari ambayo hutua kwanza kisiwani hapo laikini vilevile taa za kuongozea meli zipo kisiwani pale lakini muhimu zaidi kulika kwa kisiwa hiki kunaongeza tope katika kina cha bandari ya Tanga jambo linalotishia thamani ya bandari hiyo.
Katika mwendelezo wa ziara yake katika mkoa wa Tanga Waziri Makamba amefika katika Wilaya ya Mkinga ambapo alipokea taarifa ya mazingira ya wilaya toka kwa Mkuu wa Wilaya Yona Maki iliyoainisha changamoto mbalimbali za kimazingira katika wilaya hiyo zikiwemo uchimbaji madini karibu vyanzo vya maji, kukata na kuchoma miti katika vyanzo vya maji uchomaji mkaa kinyume na taratibu, uchomaji moto hovyo wa misitu, uharibifu wa misitu ya bahari (Mikoko) kwaajili ya kusafirisha kwenda nchi jirani ya Kenya pamoja na uvuvi haramu unaotumia baruti.
Katika kikao na mkuu wa Wilaya, Meneja misitu wa wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Frank Chambo ameeleza changamoto ya wahamia haramu toka nchi jirani ya Kenya kuvamia maeneo ya Misitu hasa Tao la Mashariki na kujishugulisha na shughuli za uharibifu wa mazingira kinyume na taratibu pamoja na sheria za nchi.
Waziri Makamba ameagiza kufanyika kwa operesheni maalum kukabiliana na wahamiaj haramu kwani si tishio kwa mzingira pekee bali ni tishio kwa usalama kwa ujumla.
Waziri Makamba amefika katika kijiji cha Segoma Kata ya Mhinduro amabapo ametembele na kukagua eneo la mto Zigi mto ambao licha ya kuwa chanzo kikuu cha maji kwa wananchi wa mkoa wa Tanga umeathiriwa kwa kiasi kikubwa na shughuli za kibinadamu hasa uchimbaji madini katika kingo zake, uchimbaji ambao sio tu unaacha mashimo katika maeneo ya mito bali pia sumu inayotumiwa katika uchimbaji inahatarisha afya za watumiaji maji ya mto huo.
Baada ya ukaguzi huo Waziri Makamba alizungumza na wanakijji katika mkutano wa hadhara ambapo alisisitiza umuhimu wa utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji.
“maendeleo yetu sisi kama watu Mkinga na watanzania kwa ujumla hayawezi kutenganishwa na hifadhi ya mazingira, hivi ni vitu vinavyofungamana kwa kiasi kikubwa hivyo ni lazima muunge mkono kwa vitendo jitihada zinazofanywa kulinda mazingira hasa vyanzo vya maji “. Alifafanua Waziri Makamba katika mkutano huo wa hadhara ambapo amewataka wananchi kuwafichua wale wote wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini kinyume na taratibu katika maeneo ya vyanzo vya maji.
Waziri Makamba amefika pia katika Kijiji cha Bosha na kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho katika mkutano wa hadhara juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira pamoja na athari za uharibifu wa mazingira. Amewataka wananchi wa Bosha kuacha mara moja kufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji ikiwemo uchimbaji wa madini katika maeneo ya vyanzo vya maji kwani kuendelea uwepo wa maisha katika kijiji hicho kwa vizazi vijavyo kwa kiasi kikubwa unategemea sana jitihada za sasa za utunzaji wa Mazingira. Pia amewataka viongozi wa kijiji kuhakikisha usimamizi wa sheria ndogo za mazingira unafanywa pamoja na kuhakikisha kamati ya mazingira ya kijiji inafanya kazi ipasavyo.
Katika kuchangia shughuli za maendeleo kijijini hapo Waziri Makamba amechangia Mifuko 30 ya sementi kwaajili ya kusaidia ujenzi wa zahanati ya kijiji unaoendelea.
TAZAMA JAMAA HUYU ALIVYOKOSWA KOSWA NA KIFO KWA AJARI MTONI
from Blogger http://ift.tt/2odGeBD
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2nvO2BJ
No comments:
Post a Comment