Seneta wa Jiji la Nairobi nchini Kenya, Mike Sonko ametoa vyeti vyake hadharani baada ya kutuhumiwa na wabunge wa Jubilee Party kuwa hana vyeti halali na hivyo chama hakiwezi kumpitisha kugombea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Sonko amevitoa vyeti hivyo halali vya elimu ya nchini Kenya ili kukata mzizi wa fitia ambao mwenyewe amedai kuwa ni njama za baadhi ya watu wanaotaka asipitishwe na chama kugombea.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Soko ameweka vyeti hivyo na kusema, ni heri akataliwe na wananchi kuliko na baadhi ya bunge ambao hawana hata uhakika wa kuchaguliwa awamu ijay0.
Mbali na vyeti vya shule alivyochapisha mtandaoni, Sonko pia ameweka nyaraka za Cheti cha Polisi, Cheti cha Kodi, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, na vyeti vingine vya chuo.
Aidha, Sonko amemwambia mpinzani wake Peter Kenneth na Mbunge wa Jimbo la Nairobi kuwa hawatakiwa kuwachagulia watu zaidi ya milioni 2 waliojiandikisha kupiga kura, badala yake wawaache wananchi wachague kiongozi wanayemtaka.
from Blogger http://ift.tt/2numHAy
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2myVIiu
No comments:
Post a Comment