Wakili Tundu Lissu ambaye anamuwakilisha mjibu rufani, Mbunge wa Bunda – Esther Bulaya ameiomba Mahakama ya Rufaa jijini Mwanza kwamba shauri hilo lihamishiwe jijini Dar es salaam. Ameiomba Mahakama kufanya hivyo kwakuwa ameshakubaliana na mawakili wa wakata rufaa juu ya jambo hilo. Pia ameomba shauri hilo lisianze kusikilizwa jana kwakuwa anahitaji muda kuisoma rufaa hiyo na kuielewa na kwamba muda wa kisheria bado unamruhusu kuwasilisha ombi hilo. “Mheshimiwa Jaji…toka Februari 11 mwaka huu, siku 30 bado,” alieleza.
Kesi hiyo ilifunguliwa na wananchi wanne wakipinga ushindi wa Bulaya katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Kesi hii ilifunguliwa na wananchi hao kwa niaba ya aliyekuwa mgombea wa ubunge wa Jimbo hilo kwa kiti cha CCM, ndugu Steven Wasira. Wapiga kura hao wanapinga maamuzi ya Mahakama Kuu Kanda ya Musoma yaliyohalalisha ushindi wa Bulaya katika Uchaguzi Mkuu uliopita.
Pia, Lissu alisema kuwa aliipata rufaa hiyo kimakosa, kosa lililofanywa na upande wa waliokata rufaa hiyo. Alisema kwa utaratibu, wakili wa upande wa wakata rufaa walipaswa kumpatia rufaa hiyo lakini hawakufanya hivyo. Hata hivyo, amesema anawasamehe kosa hilo. “Rufani hiyo nimeipata kimakosa kwani nilitumiwa na kijana mmoja, Wakili wa hapa Mwanza, hivyo nasamehe makosa hayo bila malipo,” alisema Lissu.
Kutoka kushoto: Wakili Costantine Mtalemwa, Tundu Lissu na Esther Bulaya, wakisalimiana baada ya kesi kuahirishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza
Wakili wa upande wa wakata rufaa, Constantine Mtalemwa alikubaliana na maombi yote mawili ya Tundu Lissu, lile la kuihamishia kesi hiyo jijini Dar es salaam na kupewa siku 30 ili haki itendeke.
Jamaa atengeneza ndege YAFANIKIWA KURUKA
from Blogger http://ift.tt/2mi0uRO
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2lCk5Pj
No comments:
Post a Comment