WAMAMCHI wajimbo la Ludewa wamedaiwa kuto jitokeza kupiga kura kwa wingi kutokana na kuwapo masikitiko ya kifo cha aliyekuwa wa mbunge wao Deo Filikunjombe na mambo mgengine ya Mvua.
Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi katika jimbo la Ludewa msimamizi na Mkurugenzi wa halmashauli ya Ludewa William Waziri alisema kuwa wananchi katika jimbo hilo hawajajitokeza kwa wingi kupiga kura kutokana na jimbo hilo kipatwa na msiba wa mgombea wa ubunge na aliye kuwa mbunge wao Filikunjombe.
“Wananchi wamejitokeza wachache katika uchaguzi huu kutokana na mbunge wao na aliyekuwa akigombea ubunge kufariki na kurazimiaka zoezi la uchaguzi wa ubunge kusogezwa mbele,” alisema Waziri na kuongeza
“Walio jiandikisha katika dafutari la wapiga kura katika uchaguzi huu ni watu 65238 walio piga kura ni 34914 kitu kinacho onyesha kuwa watu wengi hawajashiriki katika uchaguzi huu,” alisema Waziri.
Alimtangaza Deogratius Ngalawa kuwa ndio mshindi wa ubunge katika uchaguzi huo mdago ambapo alkipata kura 23861 dhidi ya Bathromeo Nsambichaka ambaye alipata kura 7956 kati ya kura 31994 zilizo pigwa huku kura 177 zikiharibika na kufanya kura harali kuwa 31817.
Alisema kuwa wananchi katika jimbo hilo wamekuwa na mwamko wa chini kujitokeza kwenye uchaguzi huo ulio fanyika Disemba 20 na kusababisha watu kujitokeza kwa uchache tofauti na ule uchaguzi mkuu wa Oktoba 25.
“Wananchi wa jimbo la Ludewa wamejitokiza wachache kupiga kura ni kutokana na kutokea kwa msimba ambao ulitukuta kwa kufiwa na mbunge wetu mtarajiwa na aliyekuwa mgombea, na kufanya watu wasiwe katika hali nzuri, lakini kulikuwa na hali ya mvua iliyo sababisha watu kuto jitokeza,” alisema Waziri.
Waziri amesema kuwa wananchi walio jitokeza kupiga kura katika uchaguzi huu ni wachache kupindikia kuliko walio jitokeza kwenye uchaguzi mkuu na ukilkinganisha na idadi ya watu walio jiandikisha.
Alisema kuwa wananchi wa jimbo hilo pia mvua ili sababisha wasijitokeze kwa wingi kutokana na siku ya uchakuzi kushinda mvua ina nyesha karibu nusu ya siku hiyo.
Jimbo la Ludewa lina jumla ya kata 26 huku baadhi ya kata hizo kuwa mbali na makao makuu ya halimshauri hiyo na kusababisha kutumia bodi na barabara kuzifikia kitu kilicho sababisha matokea ya jimbo hilo kuchelewa kutoka.
Matokeo katika jimbo hilo yametangazwa juzi majira ya saa mbili husuku na mgombea wa CCM Akishiriki wakati wa kutangaza matokeo hayo na wa Chadema kuto onekana katika eneo hilo.
Ngalawa wa CCM aliye tangazwa kumridhi Deo Filikunjombe amesema kuwa anakazi kubwa ya kuwabadilisha kifikira wananchi wa jimbo hilo hasa vijana, kutokana na kuwa na mawazo mgando na kuwa atakabiliana na changamoto hiyo huku toa shukrani za kutosha kwa wananchi walio msaidia kushinda.
“Jimbo la Ludewa lina changamoto moja kubwa ambayo ni kuwepo kwa vijana wenye mawazo hasi vivyo nitajitahidi kuanza na change moto hiyo kuwabadilisha mawazao yao na nitahakikisha kuwa vijana hao wanajitambua na wakinamama wanajitambua,” alisema Ngalawa.
Alisema kuwa atajitahidi kwenda na kasi ya Rais Dr. Jonh Magufuli katika kuhakikisha kuwa jimbo hilo linapata maendeleo kama alivyo kuwa akifanya Marehemu Filikunjombe.
Hata hivyo wananchi baada ya kutangazwa walishukuru kumpata mbunge chaguo lao ambaye anamridhi Mbunge wao marehemu Filikunjombe.
from Blogger http://ift.tt/1mxRAj2
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/1MtD14I
No comments:
Post a Comment