Tuesday 10 November 2015

TANGU kuanza kwa siasa za vyama vingi nchini Tanzania na kufanyika uchaguzi mku wa kisiasa kukiwa na vyama vingi mwaka 1995 kwa mara ya kwanza chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Kimepata Mbonge wa kwanza mkoani Njombe.

Chama hicho tangu kuanza kwa siasa za viama vingi kumefanikiwa kupata mbunge mmoja wa viti maalum ambaye ndio anakuwa wakwanza kuwa mbunge wa Chadema tangu kuanza kwa vyama vingi.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka jijini Dar es salamu na kupokelewa na wananchama wa chama hicho Mteuliwa viti maalumu Ubunge mkoa wa Njombe Chadema, Lusia Mlowe alisema kuwa yupo tayari kuhakikisha kuwa wakazi wa Njombe wanaona matunda ya kuwa na mbunge wa upinzani kwa kuhakikisha anasukuma maendeleo mbele licha ya kuwa viti maalumu.

Alisema kuwa kumekuwa na kawaida ya fedha za mfuko wa jimbo kuwa ni za mbunge aliyechaguliwa atahakikisha fedha hizo zinafanya kazi iliyo lengwa na kuwa zinakuwa wazi kwa wananchi kwa kile kinachofanyika kwa jimbo husika.

Mbunge huyo ambaye pia ni mkurugenzi wa kituo cha kulelea watoto yatima alisema kuwa anauchungu na maisha wananjombe ambavyo maendeleo ya mji wao kuonekana upo nyuma licha ya kuwa ni wilaya kwa muda mrefu kuliko wilaya zingine anazo ziona zimesonga kimaendeleo.

揘ashangaa wilaya ya Njombe kuwa nyuma kimaendeleo wakati ni wilaya ya mda mrefu inashindwa kuwa na maendeleo kuliko hata wilaya jirani ya Mafinga, nitahakikisha kuwa Njombe inakuw ana maendeleo ya kutosha na kuwa ya tofauti,� alisema Mlowe.

Alisema kuwa kwa kuwa yeye ni mkazi wa Njombe akiingia Bungeni atahakikisha kuwa anawatetewa wakazi wa Njombe kwa hudi na uvumba kuhakikisha kuwa jimbo hilo lina kuwa la mfano hasa ukuzingatia kuna miradi mkubwa unaotarajia kufunguliwa wa migodi ya machimbo ya mawe.

Aidha kw aupande wake mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Njombe Abuu Mtamike ambaye pia ni Diwani wa kata ya Mjimwema alisema kuwa wanafurahi kupata mbunge hiyo mmoja baada ya kupigana kwa muda mrefu na kuwa jimbo hili tangu kuanza kwa siasa za vyama vingi mkoa wilaya hiyo haijawahi kuwa na mbunge wa Chadema.

Naye katibu wa mkoa wa Njombe Chadema Alatanga Nyagawa alisema kuwa katika mkowa wa Njombe wameandika historia kubwa sana ni kwa mara ya kwanza wanakuwa na madiwani wengi zaidi na kupata mbunge kitu ambacho wao wanaona ni kikubwa sana katika siasa za mkoa wa Njombe.

from Blogger http://ift.tt/1NoPE2h
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/1PmxJPM

No comments:

Post a Comment