Thursday, 22 October 2015

BREAKING NEWS : KESI YA WAPIGA KURA KUKAKA MITA 200 YAAHIRISHWA TENA

Wakili Peter Kibatala wa upande wa mlalamikaji akitoka katika chumba cha mahakama kwenye kesi hiyo hapo jana.
Wakili wa serikali Dk.Tulia Ackson akifanya mahojiano na wanahabari jana.

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania leo imehairisha tena kesi namba 37 ya mwaka huu, ya mlalamikaji kuiomba mahakama itoe tafsiri ya kifungu cha 104 kidogo cha (1) cha Sheria ya Uchaguzi kama kinazuia ama la wananchi kukaa umbali wa mita 200 baada ya kupiga kura katika vituo
Kesi hiyo sasa itatolewa maamuzi maalum kesho saa 4 asubuhi.
Katika kesi hiyo, mawakili wa serikali wanaongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali, Dk.Tulia Ackson huku upande wa mlalamikaji ukiongozwa na Peter Kibatala.
Shauri hilo lililofunguliwa na Mgombea Ubunge Viti Maalumu Jimbo la Kilombero (Chadema), Amy Kibatala, akitaka mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya kifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Uchaguzi.

from Blogger http://ift.tt/1hXznIS
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/1PDAlbU

No comments:

Post a Comment