Akiwa anasubiria siku yake ya kutoa maelezo kuhusiana na kesi inayoendelea kumkabili ya ukwepaji kulipa kodi hakika leo Cristiano Ronaldo alikuwa na siku njema.
Ronaldo aliiongoza Ureno kuibamiza Russia bao moja kwa sifuri huku bao pekee la Ureno likiwekwa kimiani na mshambuliaji huyo katika kipindi cha kwa kwanza.
Baada ya mchezo huo kuisha kulipigwa mchezo mwingine kati ya Mexico na Newzealand ambapo hadi mchezo huo unaisha Mexico waliibuka kidedea kwa bao mbili kwa moja.
Kwa matokeo hayo ya leo Ureno na Mexico wanakuwa wanalingana alama wote wakiwa na nne nne huku nafasi ya 3 ikishikiliwa na Urusi wenye alama 3 na Newzealand wanaburuza mkia wakiwa hawana alama hata moja na sasa wameaga rasmi mashindano hayo.
from Blogger http://ift.tt/2sTl2Xa
via IFTTT
from WordPress http://ift.tt/2tQWF9N
No comments:
Post a Comment