Sunday 16 April 2017

Timu ya Kagera Sugar Yaipinga TFF Kuipa Simba Point 3, Yaandika Barua Hii

KLABU ya Soka ya Kagera imeaiandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kulalamikia maamuzi yaliyotolewa na kamati ya saa 72 kwa kuipatia pointi tatu timu ya Simba ikidaiwa wamemchezesha mchezaji mwenye kadi tatu za njano.
Braua hiyo iliyopelekwa moja kwa moja kwa Mtendaji Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa imeandikwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo Hamis Mdaki na kuelekeza malalamiko yao ya kutokubaliana na maamuzi ya kamati ya saa 72.
Hukumu ya kuipatia Simba alama hizo ilitoka jana usiku naada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Mohamed Yahya alitoa maamuzii hayo mbele ya waandishi wa habari na kusema kuwa kamati imethibitisha kuwa Mchezaji Mohamed Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano alizozipata katika michezo dhidi ya Prisons, Majimaji na African Lyon.
Hukumu hiyo imeonekana kutokukubalika kwani kamati ilishindwa kupitia ripoti za waamuzi baada ya kuonekana kutofautiana baina ya mwamuzi na kamisaa wa mchezo na kuamua kuwaita waamuzi waje kuthibitisha kama ni kweli Fakhi alipewa kadi ya njano.
Kagera wamemtaka katibu mkuu kuiangalia upya hukumu hiyo kwani wana uhakika kuwa Fakhi alikuwa na kadi mbili za njano na sio tatu kama wanazodai Simba. Katika mchezo huo wa Kagera walifanikiwa kutoka na ushindi wa goli 2-1 dhid ya Simba uliochezwa kwenye dimba la Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera.
Baaada ya maamuzi hayo Simba wamejikita kileleni zaidi wakiwa na alama 61 wakifuatiwa na Yanga wenye alama 56.

from Blogger http://ift.tt/2pi6j6X
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2ohrIs1
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2odLbuI
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2pm7Ju0
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2pmG5gE
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2piJ9gp
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2nPfCuU
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2oKSblS
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2oyyiwc
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2pjxRsr
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2oCq73w
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2nPOADW
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2pEBiX7
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2nQqSqR
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2pkOPql
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2plav5G
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2oM6CGe

No comments:

Post a Comment