Monday 3 April 2017

ASKARI KENYA AWAUA WATU WA WAWILI KATIKATI YA BARABARA

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kenya (IGP), Joseph Boinnet ameagiza uchunguzi ufanyike haraka dhidi ya mtu anayedaiwa ni Askari wa jeshi hilo aliyerekodiwa katika mkanda wa video akiwaua watu wawili waliotuhumiwa kwa uhalifu eneo la Eastleigh, Nairobi.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Kenya, Charles Owino amesema kuwa haijalishi kama mtu huyo ni polisi au la lakini anatakiwa kutambulika kutokana na tukio hilo.
Video hiyo iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia Ijumaa inamuonyesha mtu ambaye amevalia kiraia akiwa amemkamata mtuhumiwa mmoja huku mwingine akiwa amelala chini na mwili wake umetapaa damu katikati ya barabara.
Mwanaume mwingine aliyevalia sare za polisi akiwa ameshikilia silaha inayoaminika ni AK-47 anaonekana akitawanya umma uliokuwa umekusanyika kushuhudia tukio hilo lililokuwa likifanyika katikati ya barabara.
Mtu huyo aliyevalia kiraia aliwapiga risasi watuhumiwa hao walipokuwa wakijaribu kujitetea. Mtu huyo aliomba silaha nyingine na kuwapiga tena risasi watuhumiwa hao waliokuwa wamelala chini.
Haijafahamika tukio hili lilitokea lini, lakini inadaiwa kuwa watu hao waliouawa walikuwa wanaunda kundi la wahalifu na hapo walikuwa wakijipanga kufanya tukio la wizi. Kundi hilo linalofahamika kama Super Power Gang ni miongoni mwa makundi 90 yaliyotajwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kenya Disemba mwaka jana.

from Blogger http://ift.tt/2otnPoD
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2nAsDoc
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2nwlMeG
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2nAXKzV
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2nwJkQC

No comments:

Post a Comment